National News
Ufisadi Humu Nchini Umekuwa Tatizo, Koome Asema
Jaji mkuu nchini Martha Koome ameelezea kutamaushwa na ufisadi ambao bado umekithiri katika idara mbalimbali za umma, akisema ufisadi humu nchini umekuwa tatizo la kitaifa ambalo limeathiri maendeleo.
Akizungumza jmjini Mombasa wakati wa kongamano la baraza la kitaifa kuhusu utawala na haki, Jaji Koome amesema idara za haki zina jukumu kubwa la kuzuia, kuchunguza, kulinda, kusikiliza na kutoa hukumu katika kesi za ufisadi.
Jaji Koome, amesema idara ya Mahakama nchini imeanzisha mchakato wa kubuni sera za kupambana na ufisadi zitakazokamilika na kuzinduliwa rasmi mwezi Machi mwaka huu, na kwamba mapambano dhidi ya rushwa na uhalifu wa kiuchumi ni jukumu la kila mmoja.
Wakati uo huo amesema wataimarisha ushirikiano, uwezo, kuboresha mfumo wa kisheria, sera na utawala, kuimarisha ufanisi na uwajibikaji katika vita dhidi ya ufisadi.