National News
Ruto Aomboleza Kifo cha Seneta wa Baringo
Viongozi mbalimbali nchini watuma rasila zao za rambirambi kwa familia ya mwendazake Seneta wa Baringo William Cheptumo, aliyeaga dunia baada ya kuugua kwa mda mfupi katika hospitali ya Nairobi.
Wakiongozwa na rais William Ruto, viongozi hao wamemtaja mwendazake kama kiongozi mwenye maendeleo na aliyejitolea kama mtumishi wa umma kuwafanyia wananchi wake maendeleo.
Rais Ruto amemtaja mwendakazi kama kiongozi mchapa kazi huku akisema wakaazi wa kaunti ya Baringo wamepata piga kubwa kwa kuondokewa na kiongozi wao.
Kwa upande wake Spika wa Bunge la Seneti Amason Jeffah Kingi, amesema bunge la seneti limepata pigo baada ya kumpoteza kiongozi mchapa kazi ambaye alikuwa mstari wa mbele katika kuchangia hoja muhimu bungeni.
Cheptumo amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 57 baada ya kuugua kwa mda mfupi wakati akipokea matibabu katika hospitali ya Nairobi.