National News

Madzayo Kuwasilisha Mswada Bungeni Kuhusu Utata wa Ardhi Unaoendelea Kilifi Kusini

Published

on

Seneta wa kaunti ya Kilifi Stewart Madzayo analenga kuwasilisha mswada bungeni kuhusu utata wa ardhi unaendelea kuzingira wakaazi wa eneo bunge la Kilifi Kusini.

Madzayo amesema wakaazi hao hawafai kufurushwa katika ardhi zao na baadhi ya mabwenyenye wanaodai kuwa wamiliki wa ardhi hiyo, akihoji kwamba swala hilo litatuliwa.

Akizungumza katika eneo la Majengo-Kanamai kaunti ya Kilifi, Madzayo amesema baadhi ya wakaazi wa maeneo hayo wamepewa notisi ya kuondoka kwenye makazi yao, akisema swala hilo linahitaji mazungumzo.

Wakati huo huo amewakashfu maafisa wa usalama kwa kukiuka haki za kibinadamu na kuegemea upande wa mabwenyenye ili kuwahangaisha wakaazi katika ardhi yao, akisema tabia hiyo lazima ikomeshwe.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Trending

Exit mobile version