Timu ya Bandari Queens imeanza vyema msimu mpya wa Ligi ya NSL ya wanawake 2025–2026, baada ya kuicharaza Mombasa Olympic 4-0, kwenye mechi iliyopigwa katika uwanja wa shule ya msingi ya Makande, jijini Mombasa.
Bandari Queens walitawala mchezo kuanzia mwanzo, wakipata bao la kwanza dakika ya sita kupitia Chilo Chikope, aliyeunganisha krosi safi kutoka kwa nahodha Idda Atieno.
Dakika kumi baadaye, Catherine Kanga alifunga bao la pili kwa shuti kali kufuatia pasi maridadi ya Irene Namace, na kufanya matokeo kuwa 2-0 hadi mapumziko.
Kipindi cha pili kilianza kwa kasi huku Bandari wakiongeza presha zaidi. Dakika ya 55, beki wa Mombasa Olympic Vivian Okinda alijifunga katika harakati za kuokoa, na kuongeza bao la tatu kwa Bandari.
Dakika za mwisho wa mchezo, Irene Namace alihitimisha karamu ya mabao kwa kufunga bao la nne.
Kocha wa Bandari Queens, Jonathan Washe, amesema ameridhishwa na matokeo hayo, lakini ametaka kikosi chake kuboresha zaidi safu ya kiungo na mashambulizi.
“Nashukuru wachezaji wangu kwa matokeo haya mazuri wamecheza kwa maelekezo na tutaendeleza kwa mtindo huu kuelekea mechi zijazo.”
Kwa upande wa Mombasa Olympics, kocha wao Jumanne Barne amesema licha ya kipigo kizito, ana matumaini timu yake itarejea kwa nguvu katika mechi zijazo.
“Huu ulikua mtihani mkubwa kwetu na sikushangaa sana matokeo haya maanake tulipoteza wachezaji wengi mahiri msimu jana ila tutajipanga kabila ya mechi ijayo.
