Serikali imesema imeanzisha mikakati maalum ya kuwanusuru Wakenya wanaodaiwa kulaghaiwa na mawakala bandia na kujiunga na jeshi la Urusi kupigana vita dhidi ya Ukraine.
Katibu wa Idara ya Leba nchini, Shadrack Mwadime alisema serikali inashirikiana na Wizara husika pamoja na ubalozi wa taifa la Urusi ili kubaini idadi kamili ya Wakenya walioathirika na kuhakikisha wanarejeshwa nyumbani wakiwa usalama.
Akizungumza na Wanahabari mjini Mombasa, Mwadime alizitaka familia zilizoathirika na saula hilo kuwasilisha malalamishi yao kwa tasisi husika ili kuruhusi uchunguzi wa mapema kuhusu suala hilo.
Aidha, aliwaonya Wakenya kuwa waangalifu wanaposaka ajira kwenye mataifa ya Ulaya kutoka kwa mawakala au mashirika yasiotambuliwa rasmi.
Wakati huo huo, Mwadime alisema kuwa hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi ya maafisa wa serikali au mashirika binafsi watakaobainika kuhusika katika njama za ulaghai huo.
“Kwa kupitia ubalozi wetu tukiweza kupata hizi habari na wazazi wengi tayari pamoja na watu wao wa karibu ambao kwa bahati mbaya wamepatikana na hali hiyo tayari wamefika kwa ofisi za masuala ya kigeni kwa hiyo tuko na taarifa zao na ni njia gani tutaweza kuwafikia
Hata hivyo alisisitiza dhamira yake ya kulinda raia wake na kuhakikisha kuwa taratibu sahihi za ajira nje ya nchi zinafuatwa ili kuzuia matukio kama hayo ambayo yanaweza kuleta taharuki Katika siku za usoni.
Taarifa ya Mwanahabari wetu
