News
Zoezi la kutoa chanjo kung’oa nanga Julai 5

Wizara ya Afya imetangaza kampeni ya kutoa Chanjo bila malipo kote nchini katika juhudi za kukabiliana na maradhi ya ukambi, Homa ya tumbo na Surua.
Zoezi hilo la siku 10 linatarajiwa kuanza Julai 5 mwaka huu hadi Julai 14.
Afisa wa masuala ya Chanjo kaunti ya Kilifi Christine Mataza, na mwenzake wa Afya ya Umma Amos Ndenge wamesema zaidi ya watoto elfu 200 walio chini ya umri wa miaka mitano watapokea chanjo ya ukambi na Surua.
Aidha wamesema kwamba zaidi ya Chanjo elfu 200 za Homa ya Matumbo itapeyanwa kwa zaidi ya watoto elfu 600 wa kati ya miezi tisa hadi miaka 14 katika kaunti ya Kilifi.
Chanjo hizo ambazo hutolewa kila baada ya miaka mitano, mwaka huu itaendeshwa katika sehemu za masoko, na shule, kinyume na miaka ya nyuma ambapo zoezi hilo lilikuwa likitekelezwa nyumba hadi nyumba.
Homa ya tumbo husababishwa na matumizi ya maji machafu na Mazingira machafu huku Kenya ikiwa ni Taifa la tano barani Africa kuanzisha Chanjo mpya ya kukabiliana na Huma ya tumbo, ukambi na Surua barani Afrika
Taarifa ya Eric Ponda
News
Anselim, ashutumu utovu wa usalama Taita Taveta

Kaimu Spika katika bunge la kaunti ya Taita Taveta Anselim Mwadime alieleza kusikitishwa na mauaji ya mhudumu mmoja wa bodaboda aliyeuliwa na kisha pikipiki yake kuchukuliwa katika eneo la chuo kikuu cha Taita Taveta.
Mwadime alisema kuna baadhi ya abiria ambao ni wahuni hubebwa na kisha kuwashambulia wahudumu wa pikipiki hadi kuwaua au hata kutoweka na pikipiki.
Aidha, Mwadime alisema kama viongozi wa kaunti ya Taita Taveta hawataruhusu visa hivyo kuendelezwa katika kaunti hiyo.
Vilevile, Mwadime aliishinikiza idara ya usalama kwenye kaunti ya Taita Taveta kuwajibika ipasavyo ili kudhibiti visa vya utovu wa usalama katika sekta ya bodaboda na wanaohusika wakabiliwe kisheria.
“Hili jambo linafaa kufuatiliwa kwa undani. Na tunalilaani vikali sisi kama viongozi wa Taita Taveta’’ alisema Mwadime.
Taarifa ya Janet Mumbi
News
Viongozi wahimizwa kushirikiana kubuni ajira kwa vijana

Mwakilishi wa wadi ya Sabaki eneo bunge la Magarini kaunti ya Kilifi Rose Baraka alitoa wito kwa viongozi wa kaunti ya Kilifi kushirikiana na mashirika ya kijamii pamoja na wawekezaji katika kaunti ya Kilifi ili kudhibiti changamoto za ukosefu wa ajira miongoni mwa vijana.
Rose alisema hatua hiyo itasaidia pakubwa kuwaepusha vijana kujiingiza kwenye utumizi wa mihadarati sawa na uhalifu.
Akizungumza wakati wa kikao kilichowaleta pamoja maafisa wa shirika la SHOFCO pamoja na wakaazi wa Sabaki, Rose aliahidi kushirikiana na mashirika mbalimbali ya kijamii katika juhudi za kuwasadia wananchi kujiendeleza kupitia mpango wa ajira.
“Vijana ni wengi, kazi ni kidogo. Sisi kama viongozi tunastahili kutia bidii kutafuta haya mashirika ili tuangalie vijana wetu wasaidika vipi’’ alisema Rose Baraka.
Kwa upande wake Afisa wa Shirika la SHOFCO eneo la Magarini Kelvin Mtawali Karisa aliupongeza ushirikiano wa mwakilishi wa wadi huyo na shirika hilo na kuwataka vijana kujiunga kwenye makundi mbalimbali ili waweze kupata mikopo ya kujiendeleza kimaisha.
Taarifa ya Janet Mumbi