Business
Wakulima 9,500 Kwale Kunufaika na Mavuno Bora Baada ya Kupokea Mbegu za Kisasa

Wakulima zaidi ya 9,500 katika Kaunti ya kwale hasa katika maeneo kame ya Kinango na LungaLunga wanatarajia mavuno zaidi ya mahindi, pojo na kunde, kufuatia serikali ya kaunti hiyo kuwasambazia mbegu za kisasa.
Kupitia idara ya kilimo na ufugaji, wakulima hao wamepokea mbegu hizo pamoja na mbolea ya bei nafuu ili kuendeleza kilimo hasa wakati huu ambapo mvua bado zinaendelea kushuhudiwa maeneo mengi nchini.
Kufikia sasa kaunti hiyo imesambaza tani 206 za mbegu, tani zaidi ya 1,000 za mbolea ya bei nafuu pamoja na matingatinga.
Hatua hiyo inatarajiwa kuongeza mapato na kuinua uchumi wa eneo hilo.
“Sai tunatarajia mavuno zaidi kufuatia hatua ya serikali ya kaunti kutusaidia na mbegu za kisasa na mbolea ya bei nafuu
Business
Bei ya vitunguu katika masoko ya humu nchini kuongezeka

Bei ya Vitunguu katika masoko ya humu nchini huenda ikaongezeka hata zaidi kufuatia uhaba wa bidhaa hiyo.
Kufuatia hatua hiyo wafanyibiashara wa vitunguu humu nchini wamelazimika kuagiza bidhaa hiyo kutoka taifa jirani la Tanzania kufuatia kupanda kwa bei ya bidhaa hiyo.
Wakizungumza na vyombo vya habari, Wafanyibiashara hao walisema kuna uhaba mkubwa wa vitunguu jambo ambalo limefanya bei kupanda.
Kulingana na wakulima wa zao hilo, hawakupanda vitunguu kutakana na gharama ya juu ya mbegu pamoja na changamoto za mabadiliko ya hali ya anga.
Aidha walisema kuwa gharama ya Kilimo cha vitunguu imekuwa juu ikilinganishwa na mapato ya chini na ukosefu wa bei nzuri sokoni.
Taarifa ya Pauline Mwango
Business
KEMFRI kuanzisha mradi maalum wa kuzalisha mbegu za samaki

Taasisi ya utafiti wa bahari na uvuvi nchini, KEMFRI, imeanzisha mradi maalum wa kuzalisha mbegu za samaki, ili kuongeza upatikanaji wao na kuinua sekta ya uvuvi nchini.
Akizungumza jijini Mombasa, kaimu mkurugenzi mkuu wa KEMFRI, Dkt. James Mwaluma, alisema kuwa mradi huo unatekelezwa katika eneo la Shimoni kaunti ya Kwale na unalenga kuzalisha samaki wa thamani kubwa kama vile kamba, matiko, na aina nyingine ambazo upatikanaji wake ni nadra.
Dkt. Mwaluma alisema kuwa mbegu zitakazozalishwa kupitia mradi huo zitasambazwa kwa vikundi vya vijana na wanawake wanaojihusisha na shughuli za ufugaji wa samaki, ili kuwawezesha kujitegemea kiuchumi.
Aidha, aliwahimiza vijana kote nchini wakumbatie fursa zilizopo kwenye uchumi wa baharini akisema ni njia mojawapo ya kujikwamua kimaisha na kupambana na ukosefu wa ajira.
Taarifa ya Pauline Mwango