Connect with us

Sports

Viwanja Vya Kenya Kasarani, Nyayo Tayari Kwa Kipute Cha Chan

Published

on

Mawaziri wawili waziri wa Michezo Salim Mvurya na waziri wa Usalama wa ndaani Kipchumba Murkomen wamethibitisha kwa pamoja viwanja vitakavyotumika kwa mtanange wa CHAN viko tayari.

Wakizungumza baada kuzuru uga wa Kasarani wawili hao wameweka wazi ubora wa viwanja hivyo viwili huku Mvurya akifichua kwamba kazi ya kuweka kanopi katika uga wa Nyayo kwa AFCON mwaka 2027 baada ya kukamilika kwa CHAN.

Kipute hicho kinangoa nanga mwezi ujao Agosti 2 ugani Benjamin Mkapa kabila ya fainali ugani Kasarani.

Continue Reading
Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Sports

Mabondia Kutoka Vilabu Mbalimbali Nchini, Kuzindua Uhasama Mjini Mombasa

Published

on

By

Zaidi ya mabondia 180 wa kiwango cha juu kutoka vilabu 26 kote nchini wanatarajiwa kushiriki mashindano ya ndondi ya mzunguko wa pili Kenya yanayotarajiwa kuanza hii leo hadi 19 mwaka huu yatakayoandaliwa katika taasisi ya Alliance Francaise jijini Mombasa.

Miongoni mwa mabondia watakaoshiri mashindano hayo ni Bonface Mogunde wa huduma ya polisi nchini ambaye hajapoteza pambano katika uzani wake, mshindi wa dhahabu kwenye Michezo ya Afrika Edwin Okongo wa KDF mabondia wa Mombasa, Kombo Mwinyifaki na Shaffi Bakari, pia watapanda ulingoni.

Mashindano hayo yameandaliwa na chama cha Ndondi cha Kaunti ya Mombasa kwa ushirikiano na taasisi ya Alliance Française kama sehemu ya mradi wa ushirikiano wa michezo kati ya Kenya na Ufaransa uitwao Ndondi Mashinani, kwa usaidizi wa Ubalozi wa Ufaransa.

Michuano hiyo inalenga kukuza vipaji, hasa kwa wanawake na vijana, pamoja na kuandaa wawakilishi wa Mombasa kwa mashindano ya Olimpiki yajayo.

Continue Reading

Sports

Kiungo Wa Junior Stars Aldrine Kibet Ni Mali Ya Celta Vigo

Published

on

By

 Nyota wa timu ya Taifa  ya soka Harambee Stars vijana Chipukizi ‘Junior Stars’  Aldrine Kibet sasa amejiunga rasmi na kilabu ya  Celta Vigo nchini Uhispania.
Hii ni baada ya kutia Saini mkataba na klabu hiyo inayomueka Uhispania kwa misimu minne.
Kiungo huyo wa Junior Stars, ametangazwa rasmi kujiunga na Klabu hiyo  ya Celta Vigo  kwa mkataba wa miaka minne  hadi mwaka 2029.
Kibet mwenye umri wa miaka 19 anajiunga na klabu hiyo baada ya kupitia mafunzo ya mchezo wa kandanda katika Akademia ya Nasty Sports nchini Uhispania  alichojiunga nacho miaka miwili iliopita, punde tu alipomaliza masomo  yake katika shule ya Upili Ya St. Anthony Kitale nchini Kenya.
Mchezaji huyo pia amechezea Junior Stars katika mashindano ya CECAFA humu nchini na Tanzania mwaka jana na mwaka 2023 na pia kombe la bara Afrika kwa Chipukizi mwezi Mei mjini Cairo Misri.
Continue Reading

Trending