News
Utoaji Huduma wa SHA Unachangamoto, Asema Waziri wa Afra

Waziri wa Afya nchini, Deborah Barasa, amekiri kuwepo na changamoto za utoaji wa huduma za afya kupitia mfumo mpya wa bima ya afya nchini SHA.
Waziri Deborah amesema tayari wadau wa sekta ya Afya nchini kwa ushirikiana na serikali wako mbioni kuhakikisha wanashughulikia changamoto hizo ili kuwawezesha wananchi kupata huduma bora za afya kupitia SHA.
Akizungumza na Wanahabari, Waziri Deborah ameweka wazi kwamba licha ya changamoto hizo kushuhudiwa katika maeneo mbalimbali nchini mikakati bora imeidhinishwa ili kuhakikisha huduma zote za afya zinaimarishwa vyema.
Haya yamejiri baada ya hospitali za kibinafsi za zile za kidini nchini zikidai kwamba zitasitisha utoaji wa huduma za afya kupitia bima ya Afya ya SHA kuanzia siku ya Jumatatu wakisema wanadai SHA zaidi ya shilingi bilioni 30.
News
Chama cha DCP chashinikiza wakenya kupinga mswada wa fedha, 2025

Uongozi wa chama cha DCP unashinikiza wakenya kupinga mswada wa fedha wa mwaka 2025 ukidai una vipengee tata vitakavyoongeza mzigo wa ushuru kwa wakenya.
Kulingana na Naibu Kinara wa chama hicho Cleophas Malala, mswada huo hauzingatii hali ya uchumi ya wakenya ambao wanaendelea kukabiliana na gharama ya juu ya maisha.
Malala alitaja baadhi ya vipengee vinavyoibua maswali kama vile kodi mpya ya kuongezwa kwa ushuru wa VAT kwenye bidhaa za kawaida kama vile vyakula.
Akizungumza mjini Mombasa, Malala alishauri wakenya kuwa makini na kushiriki mchakato wa kuchambua mswada huo kikamilifu vile vile kutoa maoni kwa bunge kabla ya kupitishwa na kuwa sheria.
Malala alimlaumu Kinara wa chama cha ODM Raila Odinga pamoja na Rais William Ruto akidai wamezihadaa familia zilizowapoteza wapendwa wao mwaka jana wakati wa maandamano ya kupinga mswada wa fedha kwamba zingefidiwa.
Taarifa ya Joseph Jira.
News
Mamlaka ya KPA yalalamikia changamoto zinazolemaza shughuli zake.

Licha ya Bandari ya Mombasa kuendelea kurekodi matokeo bora katika utendakazi wake,mamlaka ya bandari nchini (KPA) imebainisha kwamba bado kuna changamoto zinazolemaza shughuli zake.
Akizungumza katika kikao na kamati ya bunge kuhusu ushirikiano wa kikanda, mkurugenzi mkuu wa mamlaka ya KPA, Nahodha William Ruto, alieleza kuwa changamoto hizo ni pamoja na idadi kubwa ya mashirika yanayokagua mizigo, vizuizi vya kupima uzito wa magari (weighbridges), na vizuizi vya polisi barabarani katika eneo la Kaskazini (Northern Corridor).
Kulingana na nahodha Ruto hali hiyo bado inaathiri ufanisi wa usafirishaji wa mizigo na biashara kwa ujumla.
Nahodha Ruto pia alieleza athari za ada zisizo rasmi zinazotozwa na mashirika mbalimbali, pamoja na ushuru wa CESS unaotozwa na serikali za kaunti kwa mizigo ambayo tayari imekaguliwa na kulipiwa bandarini.
Aliongeza kuwa gharama hizo za ziada zinaathiri ushindani wa Kenya kama kitovu cha biashara katika ukanda wa afrika mashariki.
Wakati uo huo, Ruto aliitaka serikali kuharakisha uboreshaji wa mifumo ya usafirishaji kwa kuongeza matumizi ya teknolojia na kuunganisha mifumo ya upimaji wa uzito wa magari kote nchini.
Kwa upande wake, kamati ya bunge kupitia kwa mwenyekiti wake, Bi. Irene Mayaka, iliahidi kwamba kamati hiyo itafuatilia kwa karibu malalamshi yaliyoibuliwa na kuhakikisha kwamba suluhu mwafaka inapatikana.
Taarifa ya mwanahabari wetu.