Connect with us

News

Shule Ya Upili Ya Serani Ndiyo Mabingwa Eneo La Mvita

Published

on

Timu ya shule ya upili ya Serani imetetea ubingwa wao wa eneo la Mvita baada ya kuwalaza Tononoka magoli 2-1 katika fainali iliyochezewa kwenye uwanja wa shule ya upili ya Khamis.

Emanuel Oroni aliwatanguliza Serani na goli la kwanza kupitia mkwaju wa penati kabla ya Ali Abdallah kusawazishia Tononoka, lakini goli lake Emanuel Ngala katika kipindi cha pili likawapa ubingwa huo.

Kulingana na kocha wa Serani Alex Shikanga ni kwamba wamekua na mazoezi kambambe kabila ya mashindano ya shule za Upili na walikua wanasubiri ushindi tu wala si kitu kingine.

“Tulikua tumejiandaa kwa ajili ya ushindi pekee tumekua na maandalizi mazuri na hivyo nilijua tuatshinda fainali hii,katika miaka mitano tumepoteza taji hili mara moja pekee.”

kwa upande wake kocha wa Shule ya Upili ya Tononoka Juma ALi Kalato amesema kwamba amesema kwamba amekubali matokeo baada ya changamoto si haba kabila ya mechi hiyo ya fainali baadhi ya wachezaji wakingonjeka.

“Nashukuru Mwenyemezi Mungu tumefika fainali na vijana wangu wamepambana kiume kwani kabila ya mechi tulikua na wagonjwa ila wamepambana inshallah tutashinda uko mbele.”

Katika upande wa wasichana Kaa Chonjo wameibuka mabingwa kwa kuwalaza Mekatitilili magoli 3-0.

Serani na  Tononoka wataiwakilisha Mvita katika ngazi ya kaunti upande wa wavulana, na Kaa Chonjo na Mekatililii wakiwakilishja upande wa wasichana.

Continue Reading
Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

News

Godhana, awataka wakaazi kutoingiza siasa miradi ya maendeleo

Published

on

By

Gavana wa kaunti ya Tana River Dhadho Godhana amewataka wenyeji wa kaunti hiyo kujiepusha na wanasiasa ambao wanaingiza siasa kwenye masuala ya maendeleo.

Godhana alisema hilo limechangia kaunti ya Tana River kusalia nyuma kimaendeleo hali ambayo itasababisha miradi mingi kuzidi kukwama.

Godhana alisema ni lazima viongozi na wenyeji wa kaunti ya Tana River washirikiane na uongozi wa kaunti ili kuafikia utekelezaji wa miradi ya maendeleo.

Wakati huo huo Godhana aliesema mradi wa Village Cluster ambao umekuwa ukipingwa ndio utakaosaidia kudhibiti changamoto ambazo zinaikumba kaunti ya Tana River.

Naye Mahat Ali Loka ambaye ni Naibu Gavana wa kaunti ya Tana River, aliwaonya wanasiasa kutoka kaunti zingine dhidi ya kuingilia siasa za kaunti hiyo huku Spika wa bunge la kaunti hiyo Osman Noor Galole, akitoa onyo kwa wafanyikazi wa umma dhidi ya kujumu la serikali ya kaunti ya Tana River.

Taarifa ya Janet Mumbi

Continue Reading

News

Mwili wapatikana baharini Shelly Beach Likoni

Published

on

By

Polisi kaunti ya Mombasa wanachunguza kisa ambapo mwili wa mwanamme ambaye hajafahamika umepatikana ukielea katika maji ya bahari hindi kwenye ufuo wa Shelly Beach eneo bunge la Likoni.

Ripoti ya polisi ilibaini kuwa mwili huo uligunduliwa na wavuvi eneo hilo, ambao walipiga ripoti katika kituo cha polisi cha Shelly Beach kuhusiana na tukio hilo.

Polisi walisema hawakubaini mara moja anakotoka mtu huyo.

Vile vile haikubainika iwapo marehemu alizama au aliuawa kabla ya mwili wake kutupwa baharini.

Polisi walisema hawajakutana na stakabadhi zozote za kumtambulisha mtu huyo huku wakiwasihi wananchi kutoa taarifa iwapo wanafahamu familia ya marehemu.

Mwili unahifadhiwa katika hifadhi ya maiti katika hospitali ya Rufaa ya Coast General Mombasa wakati uchunguzi zaidi ukiendelea.

Taarifa ya Joseph Jira

Continue Reading

Trending