Connect with us

News

Seneta Madzayo amuonya Inspekta jenerali wa Polisi.

Published

on

Seneta wa kaunti ya Kilifi Stewart Madzayo amemtaka inspekta jenerali wa polisi nchini Douglas Kanja kuhakikisha maandamano ya vijana wa rika la Gen z tarehe 25 mwezi juni 2025 hayashuhudii umwagikaji damu.

Madzayo ambaye pia ni kiongozi wa wachache katika bunge la seneti alimtaka Inspekta Kanja kuhakikisha maafisa wa polisi wanawalinda waandamanaji badala ya kuwadhuru.

Akizungumza eneo la Mzambarauni-Mtwapa eneo bunge la Kilifi Kusini, Madzayo alidokeza kuwa maandamano hayo yatakuwa ya amani akikumbusha vijana hao wa Gen Z kuhakikisha wanadumisha amani wakati wa maandamano hayo.

“Tumeskia tarehe 25 kutakuwa na maandamano ya amani, nataka kumwambia inspekta jenerali Kanja, tafadhali watoto wetu watakuwa katika maandamano ya amani kwa hivyo usijaribu hata kidogo kutumia polisi vibaya kuweza kuumiza watoto wetu”, alisema Madzayo.

Kwa upande wake mbunge wa eneo hilo Ken Chonga aliwaomba viongozi wa kanisa nchini kuombea taifa kutokana na visa vya mauaji na utekeji nyara vinavyoshuhudiwa nchini.

“Tumekuwa na changamoto kubwa sana kati ya upinzani na serikali hali ya maafa ikiingia, haya yote ambayo yanaendelea sa hii yote sababu ni siasa, langu ni kusihi kwanza kanisa tunahitaji maombi yenu”, alisistiza Chonga.

Maandamano hayo ya GEN Z yanatarajiwa kufanyika tarehe 25 mwezi juni 2025 kukumbuka vijana waliopoteza maisha wakati wa maandamano ya kupinga mswada wa fedha mwezi juni mwaka 2024.

Taarifa ya Joseph Jira

Continue Reading
Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

News

Kindiki, ataka makubaliano kati ya serikali kuu na kaunti kutekelezwa

Published

on

By

Naibu wa rais Prof. Kithure Kindiki ametaka makubaliano yote kati ya serikali za kaunti na ile ya kitaifa kutekelezwa kabla ya mwezi Disemba mwaka huu wa 2025.

Akizungumza katika makao yake ya Karen jijini Nairobi Jumatatu 23, Juni 2025, kwenye mkutano wa 27 kati ya serikali kuu na zile za kaunti kuhusu bajeti IBEC, Kindiki alisema kumekuwa na makubaliano ambayo yamekuwa hayafuatiliwi ili kutekelezwa.

Kindiki alisema serikali kuu imejitolea kuhakikisha serikali za kaunti zinafanikisha miradi mbalimbali na kuwataka maafisa wa serikali za kaunti na ile ya kitaifa kushirikiana kwa majadiliano.

Wakati huo huo alisisitiza haja ya kutafuta suluhu la matatizo yanayoathiri utendakazi wa serikali za kaunti huku akipuzilia mbali uwepo wa mzozo wowote baina ya serikali kuu na zile za kaunti.

Taarifa ya Janet Mumbi.

Continue Reading

News

Spika Teddy, adai wabunge wa kitaifa wanachangia kutimuliwa kwake ofisini

Published

on

By

Spika wa bunge la kaunti ya Kilifi Teddy Mwambire ameibua madai kwamba baadhi ya wabunge wa kitaifa kutoka kaunti ya Kilifi ndio ambao wanaendeleza njama ya kumuondoa kama spika wa bunge hilo.

Kupitia video ambayo imekuwa ikisambaa kwenye mitandao ya kijamii, Spika Mwambire alisema viongozi hao wameshirikiana na baadhi ya Wawakilishi wa wadi wa bunge la kaunti ya Kilifi ili kuhakikisha wanafanikiwa kumbandua mamlakani.

Mwambire alisema viongozi pamoja na gavana wa kaunti ya Kilifi Gedion Maitha Mung’aro wako na njama fiche ili kuhakikisha wanatimiza malengo yao ilhali hakuna sababu zozote za kimsingi.

Aidha, Mwambire alisema hadi kufikia sasa hajajua sababu kuu ambazo zinasababisha kutaka kumbandua kama Spika wa bunge la kaunti ya Kilifi.

Vilevile, alisema hatajiuzulu kama spika wa bunge la kaunti ya Kilifi na kuwakosoa wanaomtaka kuomba msamaha bila kumfahamisha makosa yake.

Taarifa ya Janet Mumbi

Continue Reading

Trending