Idara ya usalama nchini imethibitisha kwamba baadhi ya mikutano ya kisiasa inayoandaliwa nchini, wahusika wamekuwa wakikosa kuwaarifu maafisa wa usalama.
Msemaji wa idara ya polisi nchini Michael Michiri alisema hulka hiyo ndio imekuwa ikichangia kushuhudiwa kwa vurugu za kisiasa nchini hasa kwenye mikutano ya kisiasa ya mirengo ya upinzani.
Michiri alisema kuwafamisha maafisa wa usalama ili kuchukua jukumu la kutoa ulinzi kwa wananchi wanaohudhuria mikutano hiyo sio jambo gumu bila dharura kutokana kwa wanasiasa ndio changamoto kuu.
Aidha aliwarai wananchi kuwa makini wanapohudhuria mikutano hiyo ya kisiasa ili kuepuka vurugu na majeruhi huku akisema iwapo wanasiasa watawasilisha ombi lao mapema basi watapewa ulinzi kwenye mikutano yao ya kisiasa.
Taarifa ya Mwahoka Mtsumi
