Mahakama ya Kilifi inatarajiwa kutoa hukumu ya kesi ya uharibifi wa msitu wa Arabuko Sokoke inayomkabili mwanaume wa umri wa miaka 53.
Katika kesi hiyo, mshukiwa Karisa Nyamawi Katana anadaiwa kutekeleza kitendo hicho mnamo tarehe 22 mwezi Februari mwaka huu kabla ya kunaswa na maafisa wa idara ya misitu na wale wa kaunti ya Kilifi kwenye msitu huo.
Maafisa hao wa misitu walimpata mshukiwa akikata miti ili kutengeneza vinyago pamoja na vifaa vya kazi hiyo ikiwemo Shoka mbili na tezo moja na kubainika kwamba alifanya uharibifu wa thamani ya shilingi elfu 57.
Akiwa mbele ya Hakimu wa Mahakama hiyo Charles Obulutsa, mshukiwa alikubali mashtaka dhidi yake na kuagizwa kurejeshwa Mahakamani mnamo siku ya Jumatatu tarehe mbili mwezi Machi ambapo atapewa hukumu yake.
Taarifa ya Teclar Yeri
