Mahakama Kuu imekataa kutoa amri ya muda yani Conservatory Order ili kuzuia mpango wa ubinafsishaji wa taasisi za umma ikiwemo Shirika la Kenya Pipeline kufuatia ombi lililowasilishwa na Seneta wa Busia Okiya Omtatah.
Jaji wa Mahakama hiyo Lawrence Mugambi alisema haitakuwa haki kutoa amri hiyo kwani shauri hilo lilikuwa limeorodheshwa kwa ajili ya kutajwa tu.
Mahakama ilibainisha kwamba kuna masuala yanayotofautiana katika kesi hiyo, ikiwemo hoja ya suala ambalo tayari kusikilizwa na kwamba itakuwa bora zaidi iwapo suala hilo kwanza litaamuliwe kabla ya kutoa amri yoyote ya muda.
Katika kesi hiyo mlalamishi Omtatah alikuwa aliitaka Mahakama kusitishwa kwa muda mchakato wa ubinafsishaji wa taasisi za umma ikiwemo uuzaji wa hisa, akisema mchakato huo umekiuka Katiba.
Ombi hilo la Omtatah limetaja pia kuwepo na wasiwasi wa ubinafsishaji wa uwekezaji wa umma na madai ya ushawishi wa Shirika la kimataifa ya fedha (IMF) katika maamuzi ya kifedha kwa Kenya.
Taarifa ya Mwahoka Mtsumi
