Sports
Musiala Nje Kwa Miezi Minne

Mshambulizi wa Taifa la Ujerumani na kilabu ya Bayern Munich Jamaal Musiala kuwa nje kwa kipindi cha miezi moja baada ya kuvunjika kifundo cha mguu mechi ya Kombe la Dunia dhidi ya PSG ugani Mercedez Benz Stadium mwishoni mwa Jumaa.
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 22 alikutana vibaya na kipa wa PSG Giannluigi Donnaruma dakika za lala salama kipindi cha kwanza na tayari anaendelea na matibabu nchini Ujerumani akitarajiwa kufanyiwa upasuaji wiki hii.
Katibu mkuu wa kilabu ya Bayern Marx Eberl amesikitishwa na jeraha hilo akitaja ni mbaya mno kwa tineja huyo ambaye alikua ameanza kukiwasha.
Hii ina maana kiungo huyo mshambulizi atakosa mwanzo wa msimu mpya wa Bundesliga.
Sports
Harambee Stars Kundi La Kifo Kundi B.

Sports
Kiungo Wa Brenford Bryan Mbeumo Sasa Ni Mali Ya United

Baada ya vute ni kuvute ambayo imedumu kwa kipindi cha mwezi mmoja ni rasmi kwamba kilabu ya manchester United na Brenford wameafikia makubaliano ya pauni milioni 70 ya kiungo mshambulizi Bryan Mbeumo raia wa Cameroon.
Haya yanajiri baada ya ofa mara mbili ya united kukataliwa na kilabu hio kabila ya kutuma ofa ya mwisho ya pauni milioni 65 na nyongesa ya pauni milioni 5.
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 26 yuko tayari kumwaga wino mkataba wa miaka mitano baada kukubali matakwa yake binafsi.
Mbeumo anakua sajili wa pili kwa kocha mkuu Ruben Amorim baada ya ujio wa mshmabulizi Matheus Cunha.