Business
Msongamano Miritini–Jomvu Wazidisha Hasara kwa Wahudumu wa Matatu

Wahudumu wa matatu katika barabara ya kutoka kaloleni Mombasa wanasema Biashara zao zimedorora kutokana na msongamano ambao unashuhudiwa katika eneo la miritini hadi jomvu.
Kulingana na wahudumu hao masaa wanayotumia njiani ni mengi hali ambayo inawafanya kukadiria hasara bidhaa zao zikiharibika.
Wanasema wanatumia fedha nyingi kuagiza bidhaa mbalimbali ila zinaharibikia njiani kutokana na msongamano huo.
“ tuna kaa kwa zaidi ya saa tano barabarani kufuatia msongamnao wa magari hasa malori ambayo hayasongi kabisa jambo amabyo linatusababishia hasara.
“Tunnaomba aliyepewa ujenzi wa barabara hii kuikamilisha haraka iwezekanavyo.”.
Aidha wamemtaka mwanakandarasi aliyepewa ujenzi wa barabaya hiyo kuikamilisha ili kupunguza msongamano huo kwani wanategemea Biashara kujikimu kimaisha hivyo kuendelea kuchelesha kukamilishwa kwa ujenzi huo kunazidi kuwasababishia hasara.
Business
Bei ya vitunguu katika masoko ya humu nchini kuongezeka

Bei ya Vitunguu katika masoko ya humu nchini huenda ikaongezeka hata zaidi kufuatia uhaba wa bidhaa hiyo.
Kufuatia hatua hiyo wafanyibiashara wa vitunguu humu nchini wamelazimika kuagiza bidhaa hiyo kutoka taifa jirani la Tanzania kufuatia kupanda kwa bei ya bidhaa hiyo.
Wakizungumza na vyombo vya habari, Wafanyibiashara hao walisema kuna uhaba mkubwa wa vitunguu jambo ambalo limefanya bei kupanda.
Kulingana na wakulima wa zao hilo, hawakupanda vitunguu kutakana na gharama ya juu ya mbegu pamoja na changamoto za mabadiliko ya hali ya anga.
Aidha walisema kuwa gharama ya Kilimo cha vitunguu imekuwa juu ikilinganishwa na mapato ya chini na ukosefu wa bei nzuri sokoni.
Taarifa ya Pauline Mwango
Business
KEMFRI kuanzisha mradi maalum wa kuzalisha mbegu za samaki

Taasisi ya utafiti wa bahari na uvuvi nchini, KEMFRI, imeanzisha mradi maalum wa kuzalisha mbegu za samaki, ili kuongeza upatikanaji wao na kuinua sekta ya uvuvi nchini.
Akizungumza jijini Mombasa, kaimu mkurugenzi mkuu wa KEMFRI, Dkt. James Mwaluma, alisema kuwa mradi huo unatekelezwa katika eneo la Shimoni kaunti ya Kwale na unalenga kuzalisha samaki wa thamani kubwa kama vile kamba, matiko, na aina nyingine ambazo upatikanaji wake ni nadra.
Dkt. Mwaluma alisema kuwa mbegu zitakazozalishwa kupitia mradi huo zitasambazwa kwa vikundi vya vijana na wanawake wanaojihusisha na shughuli za ufugaji wa samaki, ili kuwawezesha kujitegemea kiuchumi.
Aidha, aliwahimiza vijana kote nchini wakumbatie fursa zilizopo kwenye uchumi wa baharini akisema ni njia mojawapo ya kujikwamua kimaisha na kupambana na ukosefu wa ajira.
Taarifa ya Pauline Mwango