Sports
Mbeumo United Ndiyo Chaguo Langu

Kiungo mshamabulizi wa kilabu ya Brenford na Cameroon Bryan Mbeumo ameweka wazi kuwa anapendelea kujiunga na kilabu ya Manchester United pekee msimu huu.
Mchezaji huyo ambaye alifunga magoli 20 msimu uliopita anasema hatakubali ofa kwiengineko iwapo united hawataendelea na dili hio kumpeleka Old Trafford.
Kilabu ya Manchester United wanatarajiwa kuwasilisha ofa ya pili kusaka hudumza za winga huyo,
Hii ni baada ya ofa ya kwanza ya pauni milioni 55 kukataliwa na Brenford wiki moja iliopita.
Brenford wanataka pauni milioni 60 kumwachilia mchezaji huyo nyota ambaye pia anamezewa mate na kilabu ya Tottenham Ya Uingereza.
Sports
Kilabu Ya Oklahoma City Thunder Ndiyo Mabingwa NBA

Kilabu ya Oklahoma ndiyo mabingwa wa mchezo wa mpira vikapu marekani NBA mwaka 2025 Fainali kali iliopigwa Jumapili hii.
Hii ni baada ya vijana hao kuwanyamazisha Indiana Pacers alama 103-91 katika raundi ya 7 ya mechi hizo na kaundikisha historia mpya.
Hili ni taji lao la kwanza tangu kuondoka kutoka mji Seattle mwaka 2008.
Sports
Kikosi Cha Raga Morans Wamemaliza Ya Nne Mauritius

Kikosi cha Raga wachezaji saba kila upande chipukizi Morans kimemaliza nafasi ya nne mashindano ya Bara la Afrika nchini Mauritius.
Hii ni baada ya vijana hao kupoteza fainali ya kusaka nafasi ya tatu kwa alama 21-19 dhidi ya Zimbabwe jana jioni.Mechi hiyo ilianza kwa moto vijana wa nyumbani wakichukua uongozi wa mapema 10-0 na badaye 12-0 ila Zimbabwe wakarejea kwa moto wa radi na kuzamisha matumaini ya vijana hao kumaliza tatu bora.
Vijana hao waliwazidi nguvu Nigeria alama 43-12 katika mechi ya robo fainali kabila ya kupoteza 14-12 dhidi ya Madagascar katika mechi ya nusu fainali.
Blitboks ya Afrika Kusini ndiyo waliibukia na ushindi wakitandika Madagascar alama 28-12 katika fainali iliopigwa Jumapili na sasa timu hizo mbili zinakwenda kuwakilisha Bara Afrika katika mashindano ya dunia.