Connect with us

Sports

Mashemeji Debi ni Jumapili

Published

on

Mwenyekiti wa maandalizi ya CHAN mwezi Agosti nchini Nicholas Musonye amezionya vikali mashabiki wa Afc Leopards na Gor Mahia dhidi ya vurugu ya aina yoyote siku ya Jumapili Debi la Mashemeji. Kwenye kikao na wanahabari Musonye amesema iwapo viti vitangolewa au mawe kurushwa au rabsha ya aina yoyote basi vilabu hivyo vitakua hatarini.

“Viwanja vya Nyayo na Kasarani vimekarabatiwa rasmi kwa ajili ya michuano ya CHAN natoa onyo kwa mashabiki wa Afc na Gor iwapo viti vitangolewa ama Mawe kurushwa au rabsha ya aina yoyote hawatumia Tena viwanja hivi na watapata adabu Kali mno.

Vilabu hivyo viwili vinakutana kwa mara ya kwanza msimu huu mechi ya pili ikipigwa April 14 . Afc Leopards ndio wenyeji wa mechi hiyo na tayari tiketi zimeanza kuuzwa shilingi 500 mashabiki wa kawaida na 1000 mashabiki mashuhuri.Gor Mahia wako nafasi ya tatu ligini na alama 45 wakati Afc Leopards wakiwa ya Tano alama 39.

Continue Reading
Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Sports

Klabu ya KCB yatwaa ubingwa wa Raga ya Driftwood 7s mjini Mombasa

Published

on

By

Klabu ya KCB ndiyo mabingwa wa michuano ya Raga ya wachezaji saba kila upande ya Driftwood 7s iliyofanyika mjini Mombasa.

Hii ni baada ya kuibuka na ushindi wa alama 15–14 dhidi ya klabu ya Strathmore Leos katika fainali ya kusisimua iliyochezwa kwenye Uwanja wa Mombasa Sports Club.

KCB, maarufu kama Mabenki, walianza mchezo kwa kasi na kutawala kipindi cha kwanza. Hata hivyo, Strathmore walirejea kwa nguvu kipindi cha pili na walikuwa karibu kusawazisha, lakini walikosa kwa pointi moja pekee.

Katika mechi ya kutafuta mshindi wa tatu, Kabras RFC waliibuka na ushindi wa alama 21–10 dhidi ya Nakuru RFC, na hivyo kupanda kutoka nafasi ya nne waliyoshikilia mwaka 2024.

Wakati huo huo, katika Divisheni ya Pili, Zetech Oaks waliibuka kidedea kwa kuichapa NYS Spades kwa alama 10–0, na kutwaa ubingwa bila kuruhusu bao lolote.

Continue Reading

Sports

Timu Ya Morocco ‘Atlas Lions’ Yawasili Nairobi kwa Mashindano ya CHAN

Published

on

By

Timu ya Taifa ya Morocco, maarufu kama The Atlas Lions, imewasili jijini Nairobi tayari kwa mashindano ya CHAN yatakayofanyika mwezi ujao katika viwanja vya Nyayo na Kasarani.

Kikosi hicho chenye wachezaji 25 pamoja na benchi la kiufundi kilipokelewa vyema katika uwanja wa ndege kabla ya kuelekea hotelini, tayari kwa maandalizi ya mashindano hayo.

Morocco iko katika Kundi A pamoja na wenyeji Kenya, Angola, Zambia, na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DR Congo).

Continue Reading

Trending