Sports
Martin Zubimendi Kutua Arsenal

Kilabu ya Arsenal imekubaliana na kiungo wa Real Sociadad Martin Zubimendi kuhusiana na uhamisho wa pauni milioni 51.
Raia huyo wa Uhispania mwenye umri wa miaka 26 sasa anatarajiwa kuwasili mjini London kwa vipimo vya kimatibabu baada ya kukubali kutua Emirates.
Haya yanajiri baada kuwepo kwa ripoti nchini Uhispania kwamba Real Madrid walikua wameingia kwenye kinyanganyiro cha kusaka huduma za kiungo huyo mbunifu.
Kulingana na mkali wa taarifa za Uhamisho barani ulaya Fabrizio Romano ni kwamba mchezaji huyo amekubali kuwasili London baada kukuabaliana na matakwa yake binafsi na yuko tayari kumwaga wino mkataba wa miaka mitano.
Mchezaji huyo atakua sajili wa kwanza msimu huu kwa kocha mkuu Mikel Arteta.
Sports
Sane Sasa Ni Mali Ya Galatasaray

Ni rasmi aliyekua kiungo wa Manchester cityna Bayern Munich ya Ujerumani Leroy Sane amekamilisha uhamisho wake katika kilabu ya Galatasaray ya Uturuki bila ada yoyote.
Sane mwenye umri wa miaka 30 amepasi vipimo vya kimatibabu baada ya kuwasili mjini Istanbul alipolakiwa na mshabiki wengi wa kilabu hiyo anapojiunga na mabingwa hao wa ligi ya Uturuki.
Mchezaji huyo alijiunga na Bayern Munich msimu wa mwaka 2020 akitokea Mancity kwa mkataba wa miaka mitano na amefanikiwa kufunga magoli 61 katika mechi 220 ambazo amechezea timu hio.
Kiungo huyo pia amekua nguzo muhimu kwa timu ya taifa la Ujerumani akifanikiwa kufunga magoli 14 katika mechi 70 ambazo ameshirikisha katika timu hiyo.
Sane ni miongoni mwa wachezaji walionyeshwa mlango na kilabu ya Bayern Munich kwa msimu mpya.
Sports
Harambee Starlets Kuelekea TZ Kwa Mechi Za CECAFA

Kikosi cha soka akina dada humu nchini Harambee Starlets kimeondoka mapema leo kuelekea mjini Dar es Salaam Tanzania kwa mashindano ya CECAFA baina ya mataifa Afrika ya Mashriki.
Vipusa hao chini ya kocha Beldine Odemba ilifanya mazoezi mepesi hapo jana kabila ya kukwea pipa hii leo wachezaji 23 wakisafiri ikiwa ni wachezaji wa kimataifa na wanaocheza ligi ya nyumbani.
Starlets wanafungua kampeini Jumapili dhidi ya Burundi kabila ya kumenyana na Uganda ,Sudan Kusini na badaye kumaliza na wenyeji Tanzania.
Kwa mujibu wa kocha Beldine ni kwamba amekichagua kikosi chenye ubora huku badhi ya majina makubwa yakikosekana akiwemo mshmabulizi wa Simba Queens Jentrix Shikangwa,Teresah Engesha pamoja na Mwanahalima Dogo wote wanakosekana kwenye kambi hiyo ya Starlets.
Mechi zote zinapigwa katika uwanja wa Azam Sports Complex mjini Dar es Salaam.