National News
Kocha wa Stars Ashukuru Mashabiki

Mkufunzi wa Timu ya taifa Harambee stars Benni McCarthy amesema kwamba walikutana na mpinzani Bora Gabon katika mechi ya kufuzu kombe la Dunia ugani Nyayo siku ya Jumapili.
Haya yanajiri baada ya stars kupokea kichapo Cha magoli 2-1 dhidi ya The panthers na mwalimu ana amini Gabon tayari wa kikosi Bora kuliko stars na Hilo lilionekana.
“Ni kweli tumekutana na timu Bora ambayo tayari imenjeka kwa muda sisi tumefanya mazoezi siku mbili pekee kinyume na wao.”
Kwa upande wake kocha wa Gabon Thierry myomou amesema kwamba mipango ilifanya Kazi kwani Lengo lao lilikua Moja tu kupata ushindi ama sare ugenini kwa bahati mzuri wakaondoka na ushindi.
“Tulikua na Lengo LA kushinda mechi hii kutokea mwanzo ama kama iwe vigumu tupate sare kwa bahati mzuri tumepata alama zote tatu ni furaha kwetu kwani ulikua ni mechi ngumu mbele ya mashabiki wa nyumbani.
“Hata hivyo McCarthy ameshukuru mashabiki wengi waliokitokeza kuipa msukumo stars akikiri tangu akiwa mchezaji hajaona uwanja ukiwa umefurika hivyo akitaka mailtaifa mengine barani Afrika kuiga Hilo.
“Nichukue fursa kushukuru mashabiki wameonyesha jinsi gani wana upendo kwa timu yetu inasikitisha hatujawapa tabasamu wanaporudi nyumbani ila niwahakikishie nanjenga timu ambayo itaeletea Raha mashabiki wa nyumbani siku za usoni.”
Stars kwa Sasa wanaketi nafasi ya nne kundi F wakiwa na alama sita , Ivory coast wako kileleni na alama 16 baada ya ushindi dhidi ya Gambia nayo Gabon ni ya pili na alama 15 Burundi ni ya tatu na lama 7.
National News
Chonga: Wakenya Wanaosafiri Ughaibuni Kusaka Ajira Hawazingatii Sheria za Leba

Mwenyekiti wa kamati ya Leba katika bunge la kitaifa Ken Chonga amesema baadhi ya wakenya ambao wanasafiri katika mataifa ya miliki za kiarabu kusaka ajira wamekosa kuzingatia sheria za Wizara ya Leba nchini na kuangukia mikononi mwa walaghai.
Chonga amesema ni lazima wakenya hao wachunguze mawakala wanaowasafirisha katika mataifa hayo kama wanatambulika na serikali, ndipo waingie katika mikataba ya uajiri ambayo imezingatia sheria za Leba nchini.
Akizungumza na Wanahabari mjini Kilifi, Chonga ambaye pia ni Mbunge wa Kilifi Kusini amesema ili wakenya waepuke madhila mbalimbali kutoka kwa waajiri wao katika mataifa hayo ni lazima wasafirishwe na mawakala waliosajiliwa na serikali.
Wakati huo huo amesema japo serikali iko mbioni kuhakikisha inawatafutia wakenya kazi katika mataifa ya ughaibuni ni lazima wanaosaka ajira za ughaibuni waingie katika mkataba wa uajiri kabla ya kusafiri nje ya nchi.
National News
Chibule: Visa vya Dhulma za Kijinsi Vimepungua Kilifi

Serikali ya kaunti ya Kilifi imesema visa vya dhulma za kijinsia katika kaunti hiyo vimepungua kwa kiwango kikubwa.
Kulingana na Naibu Gavana wa kaunti hiyo Flora Mbetsa Chibule, visa hivyo viliongezeka zaidi msimu wa maambukizi ya virusi vya Corona, ambapo kaunti ya Kilifi iliorodheswa nafasi ya tatu nchini baada ya kaunti ya Bungoma na Samburu.
Chibule amesema kwa sasa ni asilimia 12.3 pekee ya visa hivyo vilivyoripotiwa tofauti na asilimia 30 wakati wa maambukizi ya Corona, akisisitiza kwamba juhudi hizo zimefanikiwa kupitia ushirikiano wa jamii na wadau mbalimbali.
Kiongozi huyo amedokeza kwamba serikali ya kaunti imetoa mafunzo kwa maafisa wa kutoa ushauri nasaha ili kusaidia kupambana na visa hivyo mashinani, akisema juhudi hizo zitaendelezwa sawa na kudhibiti madhila hayo.
Wakati uo huo ameweka wazi kwamba kaunti hiyo imekamilisha ujenzi wa sehemu salama ya kuwahifadhi watoto wanaopitia dhulma za kijinsia wakati kesi zao zikiendelea Mahakamani.