Sports
Kiungo Wa Junior Stars Aldrine Kibet Ni Mali Ya Celta Vigo

Sports
Rasmi Mshambulizi wa Uswidi Alexander Sasa ni Mali ya Liverpool

Kilabu ya Liverpool wakubaliana kumsajili mshambuliaji wa Uswidi Alexander Isak kutoka Newcastle United
Liverpool wamekubaliana kumsajili mshambuliaji wa Uswidi Alexander Isak kutoka Newcastle United kwa mkataba wa muda mrefu kwa ada ya rekodi ya Uingereza inayokadiriwa kufikia pauni milioni 130 ($175 milioni), vyombo vya habari vya Sky Sports News na The Athletic viliripoti Jumapili.
Mazungumzo ya muda mrefu kuhusu dili hilo yamekuwa yakitawala dirisha la usajili la Ligi Kuu ya England, ambalo linahitimishwa Jumatatu, huku ofa ya awali ya Liverpool ya pauni milioni 110 kwa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 25 ikikataliwa mapema Agosti.
Mchezaji huyo amepasi vipimo vya kimatibabu na anatarajiwa kumwaga wino mkataba wa miaka mitano na The Reds.
Sports
KOCHA ERIK TEN HAG RAIA WA UHOLANZI APIGWA KALAMU NA BAYER LEVERKUSEN

Mkufunzi wa zamani wa Manchester United Erik Ten Hag ametimuliwa na klabu ya Bayern Leverkusen baada ya mechi tatu pekee akiinoa klabu hiyo ya taifa la Ujerumani.
Kocha huyo raia wa uholanzi aliteuliwa na klabu hiyo ya Bundesliga mwezi Mei akiichukua nafasi ya Xabi Alonso, ambaye aliondoka kuinoa Real Madrid ya uhispania.
Hata hivyo, amekuwa na mwanzo mgumu wa maisha nchini Ujerumani, akikusanya pointi moja pekee katika mechi zake mbili za mwanzo.
Leverkusen walipoteza mchezo wao wa kwanza 2-1 wakiwa nyumbani dhidi ya Hoffenheim licha ya kupata bao la mapema kupitia kwa beki wa zamani wa Liverpool, Jarell Quansah.
Hatua ya kumtimua imekuja baada ya timu hiyo kutupilia mbali uongozi wa 3-1 ugenini Jumamosi dhidi ya wachezaji 10 wa Werder Bremen na kutoka sare ya 3-3.
Akizungumza baada ya kukatishwa tamaa Jumamosi, Ten Hag aliiambia Sky: ‘Wachezaji hawako tayari tuna timu mpya na baadhi ya wachezaji hawako fiti vya kutosha kucheza. Timu haikufanya vizuri hata kidogo wakati wa hatua ya mwisho ya mchezo. Ndivyo ilivyo. Wanahitaji kuleta nguvu zaidi na kuwa fiti zaidi ili kufikia viwango vyangu.’
Hata hivyo mchezaji nyota Florian Wirtz, Jeremie Frimpong, Jonathan Tah na Granit Xhaka ni miongoni mwa wachezaji muhimu zaidi ya nusu dazeni walioondoka Leverkusen majira ya joto.