Connect with us

News

Kaunti za Tanariver na Garissa zaathiriwa zaidi na mabadiliko ya tabia nchi

Published

on

Muungano wa mashirika ya kukabilina na athari za mabadiliko ya tabia nchi chini ya mpango wa WISER KENYA umetaja kaunti za Tanariver na Garissa kama zinazoathirika mara kwa mara na mabadiliko ya tabia nchi.

Mkurugenzi wa mpango huo Phillip Omondi ambaye pia ni mwanasayasi wa masuala ya hali ya hewa, alidokeza kuwa kaunti hizo zimekuwa zikikumbwa na hali ya mafuriko na ukame kwa mda.

Akizungumza na Coco Fm, Omondi alisema kwa sasa wanaendelea na mikakati ya kuhamasisha jamii za sehemu hizo kuhusu namna ya kukabiliana na madhara hayo.

“Kaunti za Tanariver na Garissa ambako tunatekeleza mradi wa Wiser Kenya ni kaunti ambazo ziko katika hatari ya mafuriko na ukame, kwa hio serikali ya Uingereza imeunga mkono mpango huu kupitia FCDO ili tuweze kuutekeleza ili kusaidia jamii kuepukana na mabadiliko ya tabia nchi yanayokumba kaunti hizo mbili

Mkurugenzi huyo alidokeza kuwa hatua hiyo inatokana na wito wa katibu mkuu wa umoja wa mataifa António Guterres, wa kutaka ulimwengu kuhamasisha wananchi kuhusu athari za mabadiliko ya tabia nchi.

Alidokeza kuwa wanania ya kupeleka kampeni hiyo katika kaunti nyingine nchini katika siku zijazo.

Taarifa ya Joseph Jira

Continue Reading
Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

News

Mahakama ya Kilifi imetoa hukumu kwa wanaume 6 wanaokabiliwa na mashtaka ya unajisi

Published

on

By

Mahakama ya Kilifi imetoa hukumu kwa wanaume 6 wanaokabiliwa na mashtaka ya unajisi.

Hakimu wa Mahakama hiyo Ivy Wasike alimhukumu Lucky Munga na Hassan Daniel kifungo cha miaka 30 gerezani baada ya Mahakama kubaini kwamba walihusika kwa kuwatendea unyama watoto wa umri wa miaka 13 na 15.

Safari Karisa Lewa alihukumiwa kifungo cha miaka 15 gerezani kwa kumnajisi mtoto wake mwenyewe wa umri wa miaka 14 huku Eric Ruwa na Lucky Katana Kenga wakihukumiwa kifungo cha miaka 6 gerezani kwa kosa sawa na hilo.

Hata hivyo Mahakama hiyo ilimhukumu kifungo cha miaka 3 Kithi Kombe kutokana na kesi hiyo kwa mtoto wa miaka 15, japo baadaye Mahakama ikabaini kwamba mshukiwa sio baba halali wa mtoto aliyezaliwa baada ya Kithi kumnajisi mtoto huyo.

Akizungumza wakati wa vikao vya Mahakama baada ya kutoa hukumu hizo, Hakimu Wasike alisema Mahakama umezingatia ushahidi uliyotolewa Mahakamani huku akiwarai wananchi kujitenga na visawishi vibaya ili kuepuka mkono wa sheria.

Hakimu Wasike alihoji kwamba washtakiwa wa haki ya kukata rufaa dhidi ya uamuzi wa Mahakama lakini kwa kuzingatia taratibu zote za Mahakama na sheria.

Taarifa ya Teclar Yeri

Continue Reading

News

Thoya: Serikali kuu iongeze mgao wa fedha kwa sekta ya Afya

Published

on

By

Naibu gavana wa kaunti ya Mombasa Francis Thoya ametoa changamoto kwa serikali kuu kuongeza mgao wa fedha ili kufanikisha utaoji wa huduma za afya.

Akizungumza katika kaunti hiyo, Thoya alisema kuwa huduma nyingi za afya katika kaunti hiyo ya Mombasa zinakabiliwa na changamoto ya raslimali ndogo hali ambayo inakwamisha juhudi za kuwahudumia wananchi ipasavyo.

Thoya pia alitaka serikali kuhakikisha inaharakisha kuajiri wahudumu zaidi wa afya ili wenyeji wa Mombasa waweze kupata huduma bora za matibabu bila changamoto zozote.

Aidha, Thoya alisema kwamba hali ya uhaba wa wahudumu wa afya ni changamoto kuu ambayo inazuia utoaji wa huduma bora za matibabu hali inayowafanya wale wachache waliopo kufanya kazi katika mazingira magumu.

Taarifa ya Janet Mumbi

Continue Reading

Trending