Sports
Harambee Stars Kucheza CECAFA Nchini Tanzania

Timu ya Taifa ya Soka Harambee Stars kucheza taji la Cecafa ukanda wa Afrika Mashariki mjini Dar-es-Salaam Tanzania ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya Chan mwezi Agosti.
Mashindano hayo ya nchi nne yanajumuisha Kenya, Uganda,Tanzania na Sudan Kusini yakingoa nanga rasmi Julai 24-27,Stars wakifungua kampeini yao dhidi ya wenyeji Tanzania ugani Karatu Stadium kule Arusha.
Katika mashindano hayo ya siku tatu washindi wa mechi za kwanza wanakutana kwenye fainali nazo timu ambazo zinapoteza zinacheza nafasi ya tatu na nne.
Sports
Harambee Stars Kundi La Kifo Kundi B.

Sports
Kiungo Wa Brenford Bryan Mbeumo Sasa Ni Mali Ya United

Baada ya vute ni kuvute ambayo imedumu kwa kipindi cha mwezi mmoja ni rasmi kwamba kilabu ya manchester United na Brenford wameafikia makubaliano ya pauni milioni 70 ya kiungo mshambulizi Bryan Mbeumo raia wa Cameroon.
Haya yanajiri baada ya ofa mara mbili ya united kukataliwa na kilabu hio kabila ya kutuma ofa ya mwisho ya pauni milioni 65 na nyongesa ya pauni milioni 5.
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 26 yuko tayari kumwaga wino mkataba wa miaka mitano baada kukubali matakwa yake binafsi.
Mbeumo anakua sajili wa pili kwa kocha mkuu Ruben Amorim baada ya ujio wa mshmabulizi Matheus Cunha.