News
Ethekon: Uchaguzi mkuu utakuwa huru na haki, 2027

Tume huru ya uchaguzi na mipaka nchini IEBC imewahakikishia wakenya kwamba uchaguzi mkuu wa mwaka wa 2027 kutakuwa huru na wa haki kwani tume hiyo imejipanga kikamilifu.
Mwenyekiti wa Tume hiyo Erastus Ethekon aliyataka mashirika mbalimbali ya kijamii kushirikiana ili kuhakikisha uchaguzi huyo unakuwa huru na haki.
Akizunguza katika kongamano lililowaleta pamoja washikadau mbalimbali mjini Mombasa, Ethekon aliwahimiza vijana na waundaji maudhui mitandaoni kupeperusha habari za ukweli ili kuepuka taharuki miongoni mwa jamii.
“Nawahimiza baadhi yenu muwe makini hawa ambao ni Wananbloga kulingana na athari wako naye wakati wa uchaguzi na tusikubali kutumiwa vibaya kwa ajali ya michakato ya kidemokrasia,” alisema Ethekon.
Kwa upande wake Naibu Mwenyekiti wa Tume ya IEBC Fahima Abdallah alihimiza amani kwa jamii, akisema kupiga kura ni haki ya kila mkenya na ni muhimu kutekeleza suala hilo bila vurugu.
Taarifa ya Mwanahabari wetu
News
Waziri wa zamani Dalmas Otieno Afariki

Mbunge wa zamani wa eneo bunge la Rongo Dalmas Otieno ameaga dunia.
Kiongozi huyo shupavu na mweledi katika uzungumzaji, ameaga dunia Septemba 7, 2025 nyumbani kwake katika mtaa wa Kileleshwa jijini Nairobi.
Marehemu ambaye aliwahi shikilia Wizara mbalimbali nchini pamoja na taasisi za umma muhimu kuanzia utawala wa Rais wa pili nchini Hayati Daniel Arap Moi katika miaka ya 80 atakumbukwa na wengi kwa mchango wake nchini.
Taarifa za Kifo chake zimetolewa na mwanawe Eddy Otieno.
Otieno alichaguliwa kwa mara ya kwanza kuingia bungeni na kuwaakilisha eneo bunge la Rongo mnamo mwaka 1988, na kisha baadaye kuhudumu kama Waziri wa ustawi wa viwanda kati ya 1988-1991.
Mwaka wa 1991 aliteuliwa kuwa Waziri wa Leba, lakini pia akahudumu kama Waziri uchukuzi na mawasiliano chini ya utawala wa Rais Daniel Toroitich Arap Moi.
Viongozi mbalimbali wakiongozwa na Spika wa bunge la kitaifa Moses Wetangula wametaka Mwendazake kama kiongozi alichagia mengi nchini hasa suala zima la maendeleo na miswada muhimu bungeni.
Mungu ailaze roho yake pema Peponi.
Taarifa ya Eric Ponda
News
Baraza la vyombo vya habari MCK lakerwa na baadhi ya vyombo habari

Baraza la vyombo vya habari nchini MCK limeeleza kusikitishwa na hatua ya baadhi ya vyombo vya habari nchini kumwingilia rais wa chama cha mawakili LSK Faith Odhiambo baada ya kukubali kujumuishwa kwenye kamati ya kuangazia fidia kwa waathiriwa wa maandamano nchini.
MCK ilisema hatua ya Odhiambo kujumuishwa katika kamati hiyo kuhakikisha waathiriwa wa maandamano hayo wanapata haki kwa mujibu wa sheria.
Katika taarifa kwa vyombo vya habari, baraza hilo lilipongeza juhudi za vyombo vya habari kwa kuangazia kwa undani maandamano yaliyofanyika nchini na hata baadhi ya wanabari kujitokeza kutoa ushahidi mahakamani.
MCK ilisema hatua ya baadhi vyombo vya habari kukosoa mwelekeo wa Odhiambo kunaiweka LSK katika hatari ya ukosoaji zaidi, katika juhudi za kuangazia usawa kwenye maswala ya uongozi dhabiti nchini.
Taarifa ya baraza la vyombo vya habari nchini MCK.
Ilieshinikiza wakenya kufahamu kuwa chama cha LSK kinaongozwa na taasisi muhimu za umma ikiwepo idara ya mahakama, ofisi ya mkurugenzi mkuu wa mashtaka ya umma, ofisi ya mkuu wa sheria nchini vile vile tume ya malalamishi kwa vyombo vya habari.
MCK ilivitaka vyombo vya habari kumruhusu Odhiambo kuendelea kutekeleza majukumu yake bila muingilio katika kamati hiyo.
Taarifa ya Joseph Jira