Sports
City Yasajili Wachezaji Watatu

Kilabu ya Manchester City imetangaza kukamilisha uhamisho wa wachezaji watatu tayari kwa msimu mpya baada ya kukamilisha vipimo vya kimatibabu.
Wachezaji hao watatu ni pamoja na beki Rayan Ait -Nouri kutoka kilabu ya Wolves kwa pauni milioni 31 mchezaji huyo tayari amepasi vipimo vya kimatibabu na kumwaga wino mkataba wa miaka mitano na The Citizens.
Wachezaji wengine ni Tijjani Reinders ambaye amejiunga na kilabu hiyo kwa pauni milioni 55 akitokea kilabu ya AC Milan ya Italia kwa mkataba wa miaka mitano pia.
Timu hiyo pia imekamilisha usajili wa winga wa taifa la Ufaransa na kilabu ya Lyon ya Ufaransa Rayan Cherki ambaye anajiunga na kilabu hiyo kwa pauni milioni 45 na ametia wino mkataba wa miaka mitano.
Continue Reading
Sports
Manchester United Ndiyo mabingwa wa ‘PREMIERE LEAGUE SUMMER SERIES’

Manchester United imetwaa ubingwa wa kombe la ‘Premier League Summer Series’ kufuatia sare ya 2-2 dhidi ya Everton katika dimba la Mercedes-Benz, Atlanta, Georgia Marekani.
Michuano hiyo ya maandalizi ya msimu mpya ilishirikisha timu nne za Ligi Kuu England Man United, West Ham United, Everton na Bournemouth ambapo Mashetani hao Wekundu wamemaliza kileleni pointi 7 baada ya mechi tatu, wakishinda mechi mbili na kutoka sare mechi moja.
Kiungo Bruno Fernandes aliwaweka uongozini United dakika ya 18 kupitia mkwaju wa Penalti au Tuta kisha Iliman Ndiaye akisawazishia The Toffees dakika ya 40,United tena walichukua uongozi kupitia kwa kiungo mshambulizi Mason Mount dakika ya 69 kabila ya beki Ayden Heaven kujifunga dakika ya 75.
MSIMAMO:
1. Man UTD — mechi 3 — pointi 7
2. West Ham mechi 3 — pointi 6
3. Bournemouth mechi 3 — pointi 3
4. Everton mechi 3 — pointi 1
Sports
Stars yaanza vema CHAN kwa ushindi goli 1-0 dhidi ya DR-Congo

Timu ya Taifa ya Kenya (Harambee Stars) imechukua alama zote tatu kufuatia ushindi wa 1-0 dhidi ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo kwenye mchezo wa kwanza wa Kundi B wa kombe la Mataifa Afrika CHAN 2024 katika dimba la Moi Sports Centre, Nairobi.
Goli hilo la kipekee lilitiwa wavuni na kiungo mshambulizi Austine Odhiambo dakika 45 kipindi cha kwanza.
Rais William Ruto ambaye alifuatilia mechi hiyo uwanjani alitembelea kikosi katika chumba cha kubadilisha na kukabidhi ahadi yake ya shilindi milioni moja kwa kila mchezaji baada ya ushindi huo.
Stars wamekwea kileleni mwa kundi A na alama Tatu kundi ambalo pia lina Morocco,Zambia na Angola Mechi ijayo ya Stars ni dhidi ya Angola ni Agosti 7.