Connect with us

Sports

Bado Hawajamaliza Kulipa Starlets Asema Rais Wa FKF

Published

on

Rais wa Shirikisho la mchezo wa soka nchini Hussein Mohammed amefichua kwamba wamelipa badhi ya marupurupu kwa kikosi cha soka kwa akina dada Harambee Starlets.

Hata hivyo akizungumza na kituo kimoja nchini Mohammed amefichua kwamba bado hawajalipa marurupu ya kikosi hicho mechi za kirafiki dhidi ya Ivory Coast mwezi April,Rais huyo akiongezea kwamba kazi ya kulipa wachezaji hao ni ya Serikali kupitia wizara ya michezo na wala si ya Shirikisho la soka nchini.

“Tumelipa badhi ya marupurupu kulikuwepo na tatizo upande wa wizara ila swala hilo sasa limetatuliwa akina dada hao watapokea pesa zao ikiwemo ya Cecafa nchini Tanzania.”

Alipoulizwa iwapo kama ndiyo chanzo ya badhi ya wachezaji kujiondoa kwenye kambi ya Starlets Hussein amesema wanasubiri ripoti kutoka kwa kocha wa timu hiyo Beldine Odemba.

Starlets wako nchini Tanzania mashindano Afrika Mashariki na kati CECAFA.

Continue Reading
Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Sports

Kilabu Ya Kenya Police Mabingwa Ligi Kuu FKF PL

Published

on

By

Timu ya Kenya Police FC imetawazwa mabingwa wa Ligi Kuu ya FKF kwa mara ya kwanza tangu kuanzishwa kwake, katika mechi ya mwisho dhidi ya Gor Mahia iliyopigwa kwenye Uwanja wa Ulinzi Sports Complex, .

Mabingwa hao wapya walionesha ari ya kupigania hadi dakika ya mwisho, wakitoka nyuma na kupata sare ya 1–1 dhidi ya Gor Mahia waliokuwa nafasi ya pili kwenye msimamo wa ligi.
katika matokeo mengine jana:

AFC Leopards  0-0 KCB,BANDARI 1-1 POSTA,KAKAMEGA HOMEBOYZ 0-0 TUSKER,KSHARKS 4-1 MARA SUGAR,SHABANA 1-1 ULINZI STARS,MURNGA 1-0TALANTA,Shabana 1-1 Ulinzi Stars,Nairobi City Stars 0-0 Mathare United ,Sofapaka 1-2 Bidco United.

Vilabu vya Niarobi City Stars na Talanta vimeteremshwa ngazi huku Posta Rangers ikimaliza nafasi ya 16 na sasa italazimika kucheza mechi ya mchujo dhidi ya timu ya tatu ya ligi ya daraja ya pili NSL.

Continue Reading

Sports

Liverpool Yakubaliana Dili Ya Kerkez

Published

on

By

Kilabu ya Liverpool imekubaliana na AFC Bournemouth kuhusiana na uhamisho wa pauni milioni 4o kwa beki Milos Kerkez raia wa Serbia.

Tineja huyo anatarajiwa kuwasili Liverpool muda wowote kufanyiwa vipimo vya kimatibabu na kumwaga wino mkataba wa miaka mitano na mabingwa hao wa ligi kuu Uingereza.

Mchezaji huyo alikua nguzo muhimu kwa kilabu ya Bournemouth wakimaliza kumi bora akichangia magoli matano na kufunga mawili,anakua sajili wa tatu kwa kocha Arne Slot kwenye kilabu hio.

The Reds wakiwa wametumia pauni milioni 116 kumpata kiungo Florian Wirtz,pauni milioni 31 kupata Jeremie Frimpong.

Continue Reading

Trending