Connect with us

News

Mchakato wa kuwapiga msasa Makamishena waanza Bungeni

Published

on

Bunge la kitaifa limeanza kuwapiga msasa makamishena  wateule 7 wa tume ya  Uchaguzi na mipaka, IEBC katika majengo ya Bunge.

Shughuli hiyo imeanza leo Jumamosi Mei 31 2025, kufuatia maagizo ya Mahakama kuu kuondoa marufuku ya awali iliyositisha zoezi hilo.

Hata hivyo wiki iliyopita Jaji wa Mahakama hiyo Lawrence Mugambi aliliagiza bunge la kitaifa kutekeleza wajibu wake wa kikatiba wa kuwapiga msasa makamishena hao pamoja na mwenyekiti wake, ingawa ilizuia kuapishwa au kuchapishwa katika gazeti rasmi la serikali, majina ya Makamishna  wapya wa tume hiyo, hadi mchakato huo utakapokamilika .


Bunge sasa linaweza  kuendelea na zoezi la kuwapiga msasa makamishena hao 7 kufuatia uamuzi huu wa leo Mei 29 alisema Jaji mkuu  Lawrence Mugambi

Uamuzi huu ulitolewa siku chache tu baada ya mahakama hiyo kusitisha zoezi hilo la kuwapiga msasa  makamishena hao hadi pale kesi iliyokuwa imewasilishwa kotini na walalamishi wawili, Boniface Mwangi na Kelvin Roy Omondi, waliopinga uteuzi wa makamishena hao.

Makamishena hao wanaopigwa msasa ni Erastus Edung Ethekon mwenyekiti mteule,na makamishena Anne Nderitu, Moses Mukwana, Mary Karen Sorobit, Hassan Noor, Francis Odhiambo, na Fahima Abdalla,

Hii si mara ya kwanza zoezi la kuwatafuta makamishena wa IEBC kupatwa na pigo baada ya zoezi la kuwahoji watu waliopasa kuteuliwa katika nyadhifa hizo, pia kukumbwa vikwazo kufuatia kesi iliyowasilishwa mahakamani kupinga utaratibu uliodaiwa kuenda kinyume na ripoti ya NADCO ya kushirikisha maoni ya wananchi .

Continue Reading
Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

News

Kaunti ya Kilifi yajitenga na shutma za Aisha Jumwa

Published

on

By

Serikali ya kaunti ya Kilifi imejitenga na vurugu zilizoshuhudiwa wakati wa mazishi ya Afisa wa kaunti katika eneo la Msabaha wadi ya Ganda eneo bunge la Malindi siku ya Jumatatu.

Akizungumza na vyombo vya habari, Naibu gavana wa Kilifi Flora Mbetsa Chibule, alidai kwamba wanasiasa wenye malengo fiche walitumia hafla ya mazishi na kutangaza semi za uongo kuhusu msaada wa kaunti kwa familia ya mwendazake.

Chibule alitangulia kwa kuomba msamaha kwa familia ya marehemu na kukariri kuwa serikali ya kaunti kupitia gavana Gedion Mung’aro awali iliwasiliana na familia kuhusu namna ya kuipa msaada, japo haukuwekwa hadharani.

Wakati huo huo Chibule alidokeza kwamba gavana Mung’aro binasfi alitoa msaada wake wa fedha kwa familia ya marehemu.

“Huyu ni mfanyakazi wa serikali ya kaunti mbali na mstahiki gavana wetu, idara ya ugatuzi na utekelezaji ilichangia kwa mambo hayo ya mazishi, alipokuwa na anaenda kuangaliwa maisha yake kule Moshi mustahiki gavana mwenyewe alitoa nusu milioni kumsaidi Baloteli(marehemu), nilikwenda pale tukaramuka(kuomboleza) tukasema mama madamu unahii shahada tutakutafutia nafasi katika serikali ya kaunti”, alisema Chibule. 

Vile vile naibu gavana huyo aliwapa changamoto viongozi wa siasa kuheshimu hafla za mazishi na kupunguza siasa hasa wanapoalikwa katika hafla hizo.

“Jana Msabaha mfanyakazi wetu shupavu almaarufu Baloteli nikwamasikitiko makuu ya kwamba matokeo ya mazishi yale yalikwenda vile yalivyo sisi kama serikali ya kaunti tunaomba msamaha kwa familia, kwa mama Mbeyu tusamehe kwa jinsi shughuli ilivyokuwa, viongozi wenzangu tafadhali mazishi yaheshimiwe”, alisistiza naibu gavana Chibule.

Katika hafla hiyo, Mwenyekiti wa bodi ya kitaifa ya barabara Aisha Jumwa alitoa changamoto kwa viongozi wa kaunti ya Kilifi kumpa ajira mke wa Marehemu kauli ambayo iliibua hisia miongoni mwa viongozi na kusababisha rabsha.

“Nimesikiza viongozi wa kaunti hapa mmoja mpaka wa mwisho wakizungumza, sikupata hata mmoja mwenye huruma aseme Baloteli ametumikia kaunti na hivi amefariki mkewe Maurine jumatatu au jumanne ako kazini, sikusikia, lakini mimi nilikuwa nimevipanga, mmkuja matangani na kama mmempangia simzunguze kila mtu asikie, alikini kwa sababu havikuzungumiziwa nimevipatia wiki moja kama hatapata kazi nitarejea hapa maana mwanijua mimi ni mtu wa matendo”, alisema Jumwa.

Taarifa ya Joseph Jira

Continue Reading

News

Daktari Sudi, ahimiza wanaume kuzingatia mbinu za kupanga uzazi

Published

on

By

Daktari wa Afya ya uzazi katika hospitali ya Malindi kaunti ya Kilifi, Sudi Mohamed amewashinikiza wanaume katika eneo bunge la Malindi na kaunti ya Kilifi kwa jumla kuzingatia mbinu za kisasa za upangaji uzazi.

Akizungumza na Mwanahabari wetu hospitalini humo, Daktari Mohamed amesema mbinu hizo hazina madhara yoyote kwa afya ya uzazi ya wanaume.

Daktari Mohamed ameitaka jamii kuondoa dhana potofu kuhusu mbinu hizo za upangaji.

Wakati huo huo Daktari Mohamed amesema ikiwa wanaume watazingatia mbinu za upangaji uzazi itakuwa vyema kwao kwani zitawaepusha wake wao dhidi ya madhara yanayotokana na utumizi wa mbinu za upangaji uzazi.

Taarifa ya Janet Mumbi

Continue Reading

Trending