Connect with us

News

Wakaazi wa Lamu Waandamana Kupinga Mradi wa Kawi ya Mawe

Published

on

Wakaazi wa kaunti ya Lamu kwa ushirikiano na Shirika la kijamii la Save Lamu wamefanya maandamano ya amani kupinga mradi wa uzalishaji wa Kawi ya Mawe yaani Coal Plant katika kaunti hiyo.

Wakaazi hao wamesema baada ya kufanya utafiti kuhusu mradi huo wamebaini kwamba una madhara mengi kwa afya ya jamii, wakishikilia kwamba wataendelea kuupinga mradi huo wa serikali.

Wakaazi hao aidha wameitaka Mahakama ya kuu ya Malindi ambayo inatarajiwa kutoa uamuzi wake kuhusu mradi huo kusikiliza kilio cha wakaazi wa kaunti ya Lamu na kupiga marufuku ujenzi wa mradi huo.

Hata hivyo Wawekezaji wa mradi huo ambao ni Lamu Coal Power Plant wamewasilisha rufaa Mahakamani kabla ya uamuzi wa Mahakama siku ya Alhamis.

Continue Reading
Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

News

Shughuli za Masomo Zatatizwa katika Shule ya Msingi ya Arabuko Sokoke

Published

on

By

Shughuli za masomo katika shule ya msingi ya Arabuko Sokoke eneo la Kakuyuni kaunti ya Kilifi zilitatizika mapema siku ya Ijumaa baada ya Wazazi kuandamana wakilalamikia usimamizi mbaya wa shule hiyo.

Wakaazi hao wamemtaka Mwalimu kuu wa shule hiyo kupewa uhamisho kwani ameonyesha wazi kushindwa kusimamia shughuli za masomo katika shule hiyo.

Wakiongozwa na Joyce Mbuche, Wazazi hao wamesema Mwalimu mkuu wa shule hiyo amekosa kuwa wazi kwa wazazi kuhusu suala la matumizi ya Fedha ya shule hiyo pamoja na kutokuwa muadilifu kazini.

Wazazi hao hata hivyo wamesema Mwalimu mkuu huyo amekuwa hawalipi mishahara walimu ambao wanasimamiwa na wazazi katika shule hiyo huku baadhi ya wanafunzi wakikosa kusajiliwa katika mfumo wa KEMIS.

Continue Reading

News

Kuna ongezeko la visa vya wanaume kukosa nguvu za kiume eneo la Malindi

Published

on

Idara ya afya eneo bunge la Malindi kaunti ya kilifi imeripoti ongezeka la visa vya tatizo la ukosefu wa nguvu za kiume miongoni mwa wanaume katika jamii eneo hilo.

Akizungumza na Coco Fm, mtaalamu wa afya ya uzazi katika hospitali kuu ya mji wa Malindi Daktari Sudi Mohamed, amesema visa hivyo vimethibitishwa kutoka kwa baadhi ya wanaume ambao wamekuwa wakitafuta matibabu ya afya ya uzazi hospitalini humo.

Daktari Mohamed amesema hali hiyo imekuwa ikiathiri uwezo wa wanawake wengi kupata ujauzito katika jamii na hivyo kuathiri ndoa nyingi.

Aidha Daktari Mohamed amesistiza haja ya jamii kuhamasishwa zaidi kuhusu afya ya uzazi kama njia mojawapo ya kutatua tatizo la uzazi miongoni mwa wanandoa katika jamii.

Continue Reading

Trending