Connect with us

News

Tiketi za Mashemeji Debi Zimeanza Kuuzwa

Published

on

Debi la mashemeji kati ya mahasimu wa tangu jadi kilabu ya Gor Mahia na Afc leopards siku ya jumapili kuendelea kama ilivyopangwa haya ni kwa mujibu wa waandalilizi wa mtananga huo Gor.

Tiketi za mchuano huo tayari zimetolewa ambapo mashabiki wa kawaida wanalipia ada ya shilingi shs.300 na mashabiki mashuhuri shs.500.

Awali kulikua na hali ya sintofahamu kuhusiana na ubora wa uwanja wa Kasarani ambao bado unakarabatiwa kuanda mechi ila wakilishi wa kogalo wamepata hakikisho kutoka kwa wasimamizi wa uga huo.

Katika mechi ya mkondo wa kwanza timu hizo mbili ziliisha sare tasa ugani Nyayo,Kogalo kwa sasa ni ya tatu ligini na alama 51 huku Afc Leoprads wakiwa ya sita na alama 42 kutokana na mechi 29.

Continue Reading
Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

News

Arsenal Karibu Kufikia Makubaliano Mapya na Beki Gabriel

Published

on

Klabu ya Arsenal ipo katika hatua za mwisho za mazungumzo na beki wao wa kati, Gabriel Magalhães, kuhusu mkataba mpya.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 27 raia wa Brazil, bado ana mkataba unaoendelea hadi mwaka 2027, lakini klabu hiyo imekuwa ikijadiliana naye kuhusu masharti mapya ya kuboresha mkataba huo.

Ikumbukwe kuwa mazungumzo hayo yamepiga hatua kubwa, na makubaliano yanaelekea kukamilika hivi karibuni.

Taarifa hiyo inakuja kama faraja kubwa kwa The Gunners wakati wanajiandaa kwa msimu wa uhamisho wa majira ya joto, ambapo wanatarajiwa kufanya usajili muhimu ili kuimarisha kikosi.

Gabriel amekuwa mchezaji wa msingi chini ya kocha Mikel Arteta, ingawa msimu wake ulimalizika mapema mwezi Aprili kufuatia majeraha ya paja yaliyomlazimu kufanyiwa upasuaji.

Hata hivyo, beki huyo anatarajiwa kuwa fiti kabla ya msimu mpya kuanza.

Katika msimu uliomalizika wa mwaka 2024/2025, Gabriel alifunga magoli matano katika mashindano yote akiwa na Arsenal.

Continue Reading

Entertainment

#JP2025: Mavazi ya Diamond Harusini kwa Jux Yaibua Gumzo

Published

on

Msanii maarufu wa muziki kutoka Tanzania, Diamond Platnumz, ameibua mjadala mkali kwenye harusi ya kifahari ya Juma Jux na Priscilla Ojo iliyofanyika nchini Tanzania, baada ya kushindwa kufuata mavazi rasmi yaliyowekwa kwa hafla hiyo.

Alfajiri ya Alhamisi, Juma Jux alitoa ujumbe wa kukumbusha wageni wake wote kuhusu kuzingatia mavazi rasmi ya harusi hiyo: nyeusi na dhahabu.

Hata hivyo, wakati wa hafla ya mapokezi, Diamond alijitokeza akiwa amevalia suti nyeupe – akiwa ndiye mwanamume pekee aliyekiuka mwongozo wa mavazi uliotolewa.

Tukio jingine lililovutia hisia za wengi ni kutowasili kwake kwenye harusi hiyo pamoja na mpenzi wake, Zuchu.

Zuchu alifika peke yake katika hafla hiyo ya kifahari, huku Chibu Dangote (Diamond) akichelewa kufika. Hali hiyo ilizua maswali zaidi baada ya wawili hao kuketi kwenye meza tofauti, jambo lililowafanya mashabiki wao kuanza kuhusisha tukio hilo na tetesi za mgogoro kati yao.

Katika toleo la sita la harusi ya Juma Jux na Priscilla lililofanyika awali nchini Nigeria, Diamond alikuwa msimamizi mkuu (Best Man), lakini kwa hafla ya usiku iliyofanyika hivi karibuni, nafasi hiyo ilichukuliwa na msanii mwingine, Billnass.

Harusi ya Kipekee

Priscilla Ojo, binti wa muigizaji maarufu wa Nollywood Iyabo Ojo, alifunga ndoa na Juma Jux katika kile kinachotajwa kuwa mojawapo ya harusi zinazozungumziwa zaidi mwaka huu.

Sherehe hiyo, iliyopewa jina la utambulisho wa mtandaoni #JP2025, ilikuwa tamasha la kiutamaduni lililopambwa kwa shamrashamra, hisia nzito, mastaa wakuu, na mitindo ya kuvutia kutoka pande zote.

Safari ya wawili hao ilianza miezi kadhaa iliyopita, kupitia sherehe ya utambulisho iliyofanyika nchini Tanzania mwezi Februari, ambapo ndugu na marafiki wa karibu walikusanyika kushuhudia mwanzo wa safari yao ya ndoa.

Lakini Jux hakuishia hapo. Kabla ya Siku ya Wapendanao (Valentine’s Day), alifanya pendekezo jingine la ndoa, safari hii akimvisha pete ya almasi ya karati 5.2 — tukio lililowaacha wengi wakiwa na hisia kali mitandaoni, na kuthibitisha kuwa uhusiano wao umejengwa juu ya upendo wa kweli.

Baada ya hapo, wawili hao walifunga ndoa ya kiserikali (civil wedding) jijini Lagos nchini Nigeria.

Kisha, tarehe 17 Aprili 2025, Priscilla na Juma waliandaa harusi ya kitamaduni katika hoteli moja ya kifahari  iliyoko eneo la Oniru, Nigeria. Hafla hiyo ilikuwa muunganiko mzuri wa tamaduni za Nigeria na Tanzania, ambapo kila hatua ya sherehe hiyo ilikuwa na uzito wake wa kihistoria.

Jumamosi, tarehe 19 Aprili 2025, wapenzi Juma Jux na Priscilla Ojo waliidhinisha rasmi muungano wao kwa mara nyingine kupitia harusi ya kuvutia ya kanisani (white wedding) iliyofanyika jijini Lagos, Nigeria.

Msanii nyota kutoka Tanzania, Diamond Platnumz, aliteuliwa kuwa msimamizi wa harusi (Best Man), huku mwanamitindo na mshawishi wa mitandao ya kijamii, Diana Eneje, akiwa msimamizi wa bibi harusi (Best Maid).

Hafla hiyo ilihudhuriwa kwa wingi na mastaa mbalimbali kutoka tasnia ya filamu ya Nollywood na muziki, na kuwa tukio la kijamii lililoangaziwa sana na vyombo vya habari.

Miongoni mwa watangazaji wa hafla hiyo alikuwa Claudia Naisabwa kutoka Kenya. Wageni maarufu waliokuwepo pia walijumuisha Chioma Ikwokwu, Funke Akindele, rafiki wa karibu wa Priscilla Prince Enioluwa Adeoluwa kutoka Nigeria, pamoja na Raza Lee kutoka Tanzania, miongoni mwa wengine wengi waliopamba tukio hilo la kifahari.

Continue Reading

Trending