Connect with us

News

Aisha Jumwa akosolewa kutokana na matamshi yake

Published

on

Jopo la ushauri la viongozi na maimamu wa Takaungu wadi ya Mnarani kaunti ya Kilifi limeeleza kusikitishwa na kauli zilizotolewa na Aisha Jumwa kuhusiana na tukio la mauaji na maziko ya kijana mmoja eneo hilo lililomtaja kama Zakariyah Kirao Charo.

Likizungumza na vyombo vya habari, jopo hilo likiongozwa na sheikh Mahadh Ali wa msikiti Maryam limemkosoa Jumwa kwa kile lilichosema ameuhujumu uislamu kutokana na kauli alizotoa kwenye mtandao wake wa kijamii wa tiktok kuhusiana na mazishi ya kijana huyo.

Sheikh Mahadh amesema Jumwa alidai kuwa familia ya marehemu haikuhusishwa ilhali walichukua wajibu wa kuihusisha familia kabla ya hatua zozote kuchukuliwa ila wanafamilia wenyewe hawakuonyesha ushirikiano akieleza kuwa jopo hilo pia liligadhabishwa na kauli za Jumwa kuhusiana na namna mchakato mzima wa mazishi ulivyofanywa.

Akiunga mkono kauli hiyo Ustadh Mohamed Khamis amesema kwenye mkao huo kuwa amekuwa akipokea vitisho kutoka kwa Jumwa tangia mtafuruku huo ulipoanza akisisitiza haja ya swala hilo kutotumika kwa namna ya kuchochea wanajamii waislamu na wasio kuwa waislamu katika eneo hilo la Takaungu.

Aisha Jumwa /Picha kwa hisani

Ustadh Mohamed pia amekinzana na kauli kuwa marehemu alisilimishwa akiwa na matatizo ya kiakili akisema ni sharti swala hilo lisiingiziwe siasa.

Continue Reading
Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

News

Jefwa, Afikishwa Mahakamani kwa Kumjeruhi Mwanamke

Published

on

By

Mwanamume mmoja amefikishwa katika Mahakama ya Kilifi kwa kosa la kumpiga na kumjeruhi mwanamke kwa kisingizio cha uchawi.

Mahakama imearifiwa kwamba mnamo tarehe 6 mwezi Disemba mwaka 2024, mshukiwa kwa jina Jefwa Kambengu Leso, alimvamia mlalamishi Dama Mkare Lewa akiwa njiani na kumpiga hadi kumjeruhi.

Mahakama imeelezwa kwamba mshukiwa alimziba pua na mdomo mlalamishi ili kuzuia asipige kelele na kufanikiwa kutekeleza kitendo hicho katika eneo la Mdzongoloni Wadi ya Tezo katika kaunti ya Kilifi.

Hakimu wa Mahakama hiyo Charles Obulutsa, ameagiza mshukiwa wa kesi hiyo kufika Mahakamani mnamo tarehe 14 mwezi Julai mwaka huu pamoja na kuagizwa kusitisha vitisho dhidi ya mlalamishi.

Continue Reading

News

Oburu, Awakosoa Wanaopinga Ushirikiano wa Rais Ruto na Raila

Published

on

By

Seneta wa kaunti ya Siaya, Oburu Oginga amejitokeza na kutetea ushirikiano wa utendakazi kati ya Rais William Ruto na Kinara wa Chama cha ODM Raila Odinga, akisema umeunganisha sehemu ya upinzani na serikali.

Oburu amebainishwa kwamba ushirikiano huo utasaidia kufanikisha utoaji wa huduma bora kwa wakenya wote na haufai kukosolewa.

Oburu amesema viongozi ambao wanaandaa uvumi dhidi ya mpango huo wa ushirikiano wa utendakazi wana malengo mabaya ya kusambaratisha maendeleo, akiwataka kuruhusu eneo la Nyanza kunufaika kimaendeleo.

Kwa upande wake Kiongozi wa walio wachache katika bunge la kitaifa na ambaye pia ni mbunge wa Suna Mashariki Junet Mohammed amewasuta wale wanaopinga ushirikiano huo, akiwataka kupeyana nafasi kwa wakenya kunufaika kimaendeleo.

Hata hivyo Waziri wa Kawi nchini Opiyo Wandayi ameweka wazi kwamba eneo la Nyanza litaendelea kuunga mkono serikali ya Kenya kwanza kwa manufaa ya wananchi wote.

Continue Reading

Trending

Copyright © 2024 Coco Media.