News
Kilabu Ya Barcelona Yakabwa Koo UEFA

Miamba wa Uhispania kilabu ya Barcelona kina kibarua kigumu mechi ya mkondo wa pili nchini Italia baada ya kutoka sare ya magoli 3-3 dhidi ya Intermilan mechi ya mkondo wa kwanza ugani Estadio Olympic St.luis Companys siku ya jumatano.
Mshambulizi wa Ufaransa Marcus Thuram alihitaji dakika moja pekee kuwaweka uongozini vijana wa kocha Simeone Inzaghi baada ya pasi murwa kutoka kwa beki Denzil Dumfries ambaye aliongeza la pili dakika 20 badaye na kufanya mambo kuwa magoli 2-0
Hata hivyo Barcelona walikua na jambo lao wakipiga comeback ya haraka haraka kupitia winga matata tineja Lamine Yamal kunako dakika ya 24 kabla ya Ferran Torres kuweka mambo sawa dakika ya 38.
Hata hivyo licha ya kuchukua uongozi tena kupitia goli lake Denzel Dumfries dakika ya 63 The Catalans walihitaji dakika moja kusawazisha kupitia goli la kujifunga la kipa Yan Sommer baada ya mkwaju kali ilitumwa kimyani na winga wa Brazil Raphinha kunako dakika ya 64.
Mshambulizi Lamine Yamal akiwa na umri wa miaka 17 alikua anashiriki mechi yake ya 100 tangu anze kuchezea vinara hao wa Laliga.
Mechi ya mkondo wa pili itapigwa siku ya jumanne ugani San siro ambapo yeyote ana uwezo wa kupiga hatua kwenye nusu fainali hiyo.
News
Jopo la ushauri na Maimamu eneo la Takaungu lasisitiza Samuel Charo alisilimu kwa hiari yake

Jopo la ushauri na maimamu katika eneo la Takaungu wadi ya mnarani kaunti ya Kilifi limepinga madai yalioibuliwa na wanafamilia wa kijana aliyeuawa baada ya kumuua na kula matumbo ya mzee mmoja aliyekuwa ustadh aliyetambulika kama Ainen.
Kwa mujibu wa ustadh Abubakar Ratili wa masjid Answar kule Takaungu, marehemu Samuel Kirao Charo alisilimishwa na kupewa jina Zakariyah akisisitiza kuwa marehemu alisilimu kwa hiyari yake mbele ya waislam wengine kwenye msikiti huo
Aidha Sheikh Mahadh Ali ambaye pia ni imam wa msikiti Maryam eneo hilo la Takaungu pamoja na Ustadh Mohamed Khamis wameeleza kuwa dini ya kiislam inaruhusu mwili kuzikwa usiku akikashifu swala la kuhusisha hatua hiyo na ushirikina kama ilivyodaiwa na baadhi ya watu.
Jopo hilo pia limeeleza kuwa wanafamilia walihusishwa ila walidinda kushirikiana nao jambo lililopelekea jamii hiyo ya kiislamu kuendeleza maziko ya marehemu kwa mujibu wa Imani ya dini ya kiislam.
News
Wanaharakati na vijana wa Gen -z wazua purukushani kwenye majengo ya bunge la Mombasa
Wanaharakati wa kutetea haki za kibinadamu na vijana wa Gen – Z katika kaunti ya Mombasa wemezuiwa kuingia katika bunge la kaunti ya Mombasa kuwasilisha malalamishi yao kuhusiana na bajeti ya mwaka wa kifedha wa 2025/26.
Vijana hao pamoja na wanaharakati hao waliojawa na hasira wanasema wenyeji wa Mombasa hawajahusishwa kiukamilifu Katika mchakato huo tofauti na inavyofanyika kwenye kaunti zingine nchini.
Wanadai hali ya kutokuwa na uwazi katika utekelezaji wa miswada ya fedha kwenye kaunti hiyo kunachangia kwa shughuli mbalimbali kaunti ya Mombasa kukosa kutekelezwa ipasavyo
Hatahivyo baadae Karani wa bunge la kaunti ya Mombasa salim Juma alipokea malalamishi yao na kuahidi kutoa mwelekeo ufaao Jumanne wiki ijao huku vijana hao wakitishia kurudi tena iwapo malalamishi yao hayatatiliwa maanani.

Bunge la kaunti ya Mombasa/Picha kwa hisani