News
Rais Mstaafu Uhuru Kenyatta awataka vijana barani afrika kudumisha amani

Rais Mstaafu Uhuru Kenyatta ametoa wito kwa vijana katika bara hili la afrika kuwa katika mstari wa mbele katika kuhakikisha kwamba kuna umoja kwenye bara hili.
Kenyatta ambaye alikuwa akizungumza katika Kongamano la kila mwaka la viongozi wa vyama kwenye chuo kikuu cha Makere nchini Uganda amesema kuna umuhimu wa vijana kuchukua nafasi yao katika jamii na kuliongoza bara hili la Afrika.
Aidha, Kenyatta amesema vijana wana mchango mkubwa zaidi katika kuliimarisha bara hili na kusisitiza hoja ya kuondolewa kwa vikwazo vya kibiashara baina ya mataifa ya bara la Afrika ili kuimarisha sekta hiyo.

Picha kwa hisani | Rais mstaafu Uhuru Kenyatta akisalimiana na rais wa Uganda Yoweri Kaguta Mseveni
Vilevile, Kenyatta ametoa wito kwa wadau mbalimbali barani Afrika kuendelea kuangazia uvumbuzi kama njia mojawapo ya kuimarisha maisha ya vijana ili kuwaepusha na vishawishi ambavyo vinaweza kuwafanya kupotoka kimaadili.
News
Nyakang’o, apendekeza mgao wa shilingi bilioni 1.6

Mdhibiti wa bajeti nchin Margaret Nyakang’o amependekeza kuongezwa kwa kiwango cha bajeti ya ofisi yake kutoka shilingi milioni 7.2 hadi shilingi bilioni 1.6 ili kufanikisha majukumu yake.
Akizunguza mjini Mombasa wakati wa kikao na kamati ya uekezaji wa umma na hazina maalum katika bunge la Seneti, Nyakang’o amesema bajeti hiyo ya ofisi yake iko chini mno katika kufanikisha mikakati endelevu ya majukumu yake ya kikazi.
Hata hivyo amesema iwapo bajeti hiyo itaongezwa ofisi yake itakuwa na wakati mwafaka wa kukagua miradi ya maendeleo katika kaunti zote nchini.
News
Gavana Mung’aro afanya kikao na Gach Group kuhusu uekezaji wa Madini

Gavana wa kaunti ya Kilifi Gedion Mung’aro amefanya kikao cha mazungumzo na waekezaji kutoka Kampuni ya Gach Group kuhusu uekezaji wa madini katika eneo la Magarini utakavyochangia pato la kaunti.
Kulingana na Gavana Mung’aro, uwekezaji huo utafungua nafasi za ajira kwa zaidi ya watu 500 wa eneo bunge la Magarini na kaunti ya Kilifi kwa jumla kwani waekezaji hao wanalenga madini ya Titanium na lime.
Gavana Mung’aro ameweka wazi kwamba serikali yake imejitolea kuweka mazingira bora kwa waekezaji sawa na kufanikisha mpango endelevu wa kibiashara utakaowanufaisha wenyeji.
Akizungumza baada ya kukutana na waekezaji hao kutoka taifa la Gambia, Gavana Mung’aro amedokeza kwamba kaunti ya Kilifi iko tayari kushirikiana na waekezaji wenye malengo bora kwa wananchi ili kufanikisha maendeleo.
Hata hivyo viongozi waliohudhuria kikao hicho ni pamoja na Mwenyekiti wa Gach Group Dkt Abubakar Jawara, aliyekuwa Mbunge wa Magarini Harrison Kombe, aliyekuwa Seneta wa Samburu Sammy Leshore pamoja na viongozi wengine wa kaunti.