News
KOMESHA MALARIA: Ulimwengu Waadhimisha Siku Ya Malaria Duniani

Leo ni siku ya Malaria Duniani. Katika siku hii wizara ya Afya imeandaa hafla ya hamasisho linatolewa kuhusiana na juhudi za kuudhibiti kabisa ugonjwa huu hatari hasa Katika mataifa yaliyoko kusini Mwa jangwa la Sahara.
Kenya ni miongoni wa mataifa yaliyopiga hatua kubwa katika kupambana na ugonjwa huu kupitia ushirikiano na programu za mashirika mbali mbali. Katika Kauti ya Kilifi, wizara ya afya ya kaunti ya Kilifi imeandaa maadhimisho haya katika uwanja wa Juma Chando, Banda ra Salama Chasimba – Chonyi.
Kauli mbiu ni Sisi Ndani Mbu Nje wakikokoteza utumiaji wa vyandarua ambavyo wizara hiyo na wadau wengine imekuwa ikotoa kwa wananchi.
Eneo hili ni moja ya maeneo yaliyo na maambukizo makubwa katika kaunti ya Kilifi.
News
Ruku: Serikali kuajiri vijana laki moja kwa NYS

Serikali inalenga kuajiri zaidi ya vijana laki moja katika Shirika la huduma kwa vijana wa taifa NYS.
Waziri wa utumishi wa umma nchini Geoffrey Ruku amesema hatua hiyo itachangia kuboreshwa kwa huduma za umma sawa na kuhakikisha Shirika la NYS linakuwa nguzo muhimu kwa maendeleo ya taifa.
Akizungumza katika kaunti ya Machakos, Waziri Ruku amesema hatua hiyo itapunguza utegemeaji wa ufadhili wa umma kwani shirika hilo itapanua mikakati bora ya serikali ya kibiashara pamoja na kufanikisha utoaji wa huduma kwa wananchi.
Waziri Ruku amelishinikiza bunge la kitaifa kuharakisha marekebisho ya mswada wa NYS ambao utawalishwa na Wizara yake bungeni ili kusawazisha mfumo wa kisheria wa shirika hilo.
Wakati huo huo amewataka vijana kukumbatia mipango ya serikali ya kujumuisha wananchi wote pamoja katika kufanikisha ajenda ya serikali ya maendeleo endelevu hadi mashinani.
News
Nyakang’o, apendekeza mgao wa shilingi bilioni 1.6

Mdhibiti wa bajeti nchin Margaret Nyakang’o amependekeza kuongezwa kwa kiwango cha bajeti ya ofisi yake kutoka shilingi milioni 7.2 hadi shilingi bilioni 1.6 ili kufanikisha majukumu yake.
Akizunguza mjini Mombasa wakati wa kikao na kamati ya uekezaji wa umma na hazina maalum katika bunge la Seneti, Nyakang’o amesema bajeti hiyo ya ofisi yake iko chini mno katika kufanikisha mikakati endelevu ya majukumu yake ya kikazi.
Hata hivyo amesema iwapo bajeti hiyo itaongezwa ofisi yake itakuwa na wakati mwafaka wa kukagua miradi ya maendeleo katika kaunti zote nchini.