Connect with us

National News

Usalama Waimarishwa Mombasa Mfungo wa Ramadhan

Published

on

Kamishna wa kaunti ya Mombasa Mohammed Noor amewahakikishia waumini wa dini ya kiislamu na wakaazi wa kaunti ya Mombasa usalama wa kutosha wakati huu wa mfungo wa Ramadhan.

Noor amesema idara ya usalama katika kaunti hiyo imeongeza idadi ya maafisa wa usalama ambao wanashika doria nyakati za usiku hususan katika maeneo ya Likoni na Kisauni yanayotambulika zaidi kwa visa vya utovu wa usalama.

Aidha amewataka wakaazi kushirikiana na maafisa wa usalama katika kutoa taarifa za usalama.

Kwa upande wake Gavana wa Mombasa Abdulswamad Sharif Nassir amesema serikali ya kaunti hiyo imeweka taa za mtaani maarufu Street lights ili kuhakikisha usalama unaimarishwa.

Kauli za wawili hao zinajiri baada ya kushuhudiwa ongezeko la magenge ya kihalifu yanayowahangaisha wakaazi nyakati za usiku na alfajiri.

Continue Reading
Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

National News

Chonga: Wakenya Wanaosafiri Ughaibuni Kusaka Ajira Hawazingatii Sheria za Leba

Published

on

By

Mwenyekiti wa kamati ya Leba katika bunge la kitaifa Ken Chonga amesema baadhi ya wakenya ambao wanasafiri katika mataifa ya miliki za kiarabu kusaka ajira wamekosa kuzingatia sheria za Wizara ya Leba nchini na kuangukia mikononi mwa walaghai.

Chonga amesema ni lazima wakenya hao wachunguze mawakala wanaowasafirisha katika mataifa hayo kama wanatambulika na serikali, ndipo waingie katika mikataba ya uajiri ambayo imezingatia sheria za Leba nchini.

Akizungumza na Wanahabari mjini Kilifi, Chonga ambaye pia ni Mbunge wa Kilifi Kusini amesema ili wakenya waepuke madhila mbalimbali kutoka kwa waajiri wao katika mataifa hayo ni lazima wasafirishwe na mawakala waliosajiliwa na serikali.

Wakati huo huo amesema japo serikali iko mbioni kuhakikisha inawatafutia wakenya kazi katika mataifa ya ughaibuni ni lazima wanaosaka ajira za ughaibuni waingie katika mkataba wa uajiri kabla ya kusafiri nje ya nchi.

Continue Reading

National News

Chibule: Visa vya Dhulma za Kijinsi Vimepungua Kilifi

Published

on

Serikali ya kaunti ya Kilifi imesema visa vya dhulma za kijinsia katika kaunti hiyo vimepungua kwa kiwango kikubwa.

Kulingana na Naibu Gavana wa kaunti hiyo Flora Mbetsa Chibule, visa hivyo viliongezeka zaidi msimu wa maambukizi ya virusi vya Corona, ambapo kaunti ya Kilifi iliorodheswa nafasi ya tatu nchini baada ya kaunti ya Bungoma na Samburu.

Chibule amesema kwa sasa ni asilimia 12.3 pekee ya visa hivyo vilivyoripotiwa tofauti na asilimia 30 wakati wa maambukizi ya Corona, akisisitiza kwamba juhudi hizo zimefanikiwa kupitia ushirikiano wa jamii na wadau mbalimbali.

Kiongozi huyo amedokeza kwamba serikali ya kaunti imetoa mafunzo kwa maafisa wa kutoa ushauri nasaha ili kusaidia kupambana na visa hivyo mashinani, akisema juhudi hizo zitaendelezwa sawa na kudhibiti madhila hayo.

Wakati uo huo ameweka wazi kwamba kaunti hiyo imekamilisha ujenzi wa sehemu salama ya kuwahifadhi watoto wanaopitia dhulma za kijinsia wakati kesi zao zikiendelea Mahakamani.

Continue Reading

Trending

Copyright © 2024 Coco Media.