News
Oscar Nzai Apongeza Ushirikiano wa Utendakazi Kati ya Ruto na Raila Odinga

Mwanasiasa Oscar Nzai amepongeza ushirikiano wa utendakazi kati ya Rais William Ruto na Kinara wa chama cha ODM Raila Odinga, akisema ushirikiano huo utazikabili changamoto zinazowakumba wakenya.
Nzai amesema wakenya walikuwa wakilalamika kwamba wanapitia gharama ya juu ya maisha na kumshinikiza Odinga kutatua swala hilo kama mtetezi wao lakini utetezi huo hauezifanyika kama Odinga atakuwa nje ya serikali.
Katika kikao na Wanahabari, Nzai amesema njia pekee ya Odinga kuwaokoa wakenya kutokana changamoto mbalimbali nchini, ni kupitia ushirikiano wa utendakazi na Rais Ruto huku akiwarai wananchi kuwa na subra.
“Watu wanasema kwamba Raia amekuwa akiwatetea akiwa nje lakini kuna umuhimu wa Raila kuwa ndani ya serikali iliwatetee kutoka ndani kwa sababu kwamba tunalia sisi tunasema SHA ina matatizo na tunategemea kwamba Raila ndio mtetezi wetu kwa hivyo hapo nakuna dhambi kuna manufaa makubwa zaidi”, alisema Nzai.
Wakati uo huo Mwanasiasa huyo amewaria viongozi wanaohusika na mpango wa bima ya afya ya SHA kuhakikisha wanarekebisha changamoto zinazoshuhudiwa katika bima hiyo ili kurahisisha upatikanaji wa huduma za afya.
News
Ruku: Serikali kuajiri vijana laki moja kwa NYS

Serikali inalenga kuajiri zaidi ya vijana laki moja katika Shirika la huduma kwa vijana wa taifa NYS.
Waziri wa utumishi wa umma nchini Geoffrey Ruku amesema hatua hiyo itachangia kuboreshwa kwa huduma za umma sawa na kuhakikisha Shirika la NYS linakuwa nguzo muhimu kwa maendeleo ya taifa.
Akizungumza katika kaunti ya Machakos, Waziri Ruku amesema hatua hiyo itapunguza utegemeaji wa ufadhili wa umma kwani shirika hilo itapanua mikakati bora ya serikali ya kibiashara pamoja na kufanikisha utoaji wa huduma kwa wananchi.
Waziri Ruku amelishinikiza bunge la kitaifa kuharakisha marekebisho ya mswada wa NYS ambao utawalishwa na Wizara yake bungeni ili kusawazisha mfumo wa kisheria wa shirika hilo.
Wakati huo huo amewataka vijana kukumbatia mipango ya serikali ya kujumuisha wananchi wote pamoja katika kufanikisha ajenda ya serikali ya maendeleo endelevu hadi mashinani.
News
Nyakang’o, apendekeza mgao wa shilingi bilioni 1.6

Mdhibiti wa bajeti nchin Margaret Nyakang’o amependekeza kuongezwa kwa kiwango cha bajeti ya ofisi yake kutoka shilingi milioni 7.2 hadi shilingi bilioni 1.6 ili kufanikisha majukumu yake.
Akizunguza mjini Mombasa wakati wa kikao na kamati ya uekezaji wa umma na hazina maalum katika bunge la Seneti, Nyakang’o amesema bajeti hiyo ya ofisi yake iko chini mno katika kufanikisha mikakati endelevu ya majukumu yake ya kikazi.
Hata hivyo amesema iwapo bajeti hiyo itaongezwa ofisi yake itakuwa na wakati mwafaka wa kukagua miradi ya maendeleo katika kaunti zote nchini.