News
Boresheni Vyuo vya Kiufundi, Jacinta Fondo

Serikali ya kaunti ya Kilifi imehimizwa kuboresha vyuo vya kiufundi vya TVET ili kuviwezesha kutoa mafunzo ya hadhi ya juu kwa wanafunzi.
Kulingana na Kiongozi wa vijana katika kaunti ya Kilifi Jacinta Fondo, imekuwa ngumu kwa vijana wanaofuzu kwenye vyuo vya kiufundi vya kaunti ya Kilifi kupata kazi kutokana na ukosefu wa ufahamu wa baadhi ya matumizi wa vifaa vya kisasa.
Jacinta amesema kampuni nyingi huenda zikakosa kuwaajiri vijana wanaotoka kwenye vyuo vya TVETs vya Kilifii kwani hawana uzoefu wa kutumia vifaa vya kisasa.
Wakati huo huo amependekeza serikali ya kaunti ya Kilifi kubuni ajira kwa vijana ili wanapofuzu wasitaabike kutafuta kazi.
News
Ruku: Serikali kuajiri vijana laki moja kwa NYS

Serikali inalenga kuajiri zaidi ya vijana laki moja katika Shirika la huduma kwa vijana wa taifa NYS.
Waziri wa utumishi wa umma nchini Geoffrey Ruku amesema hatua hiyo itachangia kuboreshwa kwa huduma za umma sawa na kuhakikisha Shirika la NYS linakuwa nguzo muhimu kwa maendeleo ya taifa.
Akizungumza katika kaunti ya Machakos, Waziri Ruku amesema hatua hiyo itapunguza utegemeaji wa ufadhili wa umma kwani shirika hilo itapanua mikakati bora ya serikali ya kibiashara pamoja na kufanikisha utoaji wa huduma kwa wananchi.
Waziri Ruku amelishinikiza bunge la kitaifa kuharakisha marekebisho ya mswada wa NYS ambao utawalishwa na Wizara yake bungeni ili kusawazisha mfumo wa kisheria wa shirika hilo.
Wakati huo huo amewataka vijana kukumbatia mipango ya serikali ya kujumuisha wananchi wote pamoja katika kufanikisha ajenda ya serikali ya maendeleo endelevu hadi mashinani.
News
Nyakang’o, apendekeza mgao wa shilingi bilioni 1.6

Mdhibiti wa bajeti nchin Margaret Nyakang’o amependekeza kuongezwa kwa kiwango cha bajeti ya ofisi yake kutoka shilingi milioni 7.2 hadi shilingi bilioni 1.6 ili kufanikisha majukumu yake.
Akizunguza mjini Mombasa wakati wa kikao na kamati ya uekezaji wa umma na hazina maalum katika bunge la Seneti, Nyakang’o amesema bajeti hiyo ya ofisi yake iko chini mno katika kufanikisha mikakati endelevu ya majukumu yake ya kikazi.
Hata hivyo amesema iwapo bajeti hiyo itaongezwa ofisi yake itakuwa na wakati mwafaka wa kukagua miradi ya maendeleo katika kaunti zote nchini.