Entertainment
What Is Nyevu? Magwaya, Deal na Mihangaiko Yako Tafadhali~Kelechi Afrikana
💥 Ujumbe wa mafumbo, mkorogo, na mzaha wa ‘something wet’ waunda kisanga cha kitaa!

Msanii maarufu wa R&B kutoka Pwani, Kelechi Afrikana, hatimaye amevunja ukimya wake – lakini si kwa kuachia wimbo. Badala yake, alichagua kujibu post ya muunda maudhui Nyevu Fondo kwa njia ya fumbo lenye uzito wa hisia, ladha ya ucheshi, na dongo lililotupwa kwa ustadi wa kisanaa.
Kwa mtindo wake wa kipekee, aliandika mistari iliyobeba mafumbo mazito lakini yaliyopenya kwa wepesi miongoni mwa mashabiki: “Kuna mshangazi umemshinda Magwaya Ndani. Naona unataka niletea lawama. Magwaya, deal na mihangaiko yako tafadhali.”
Hapo ndipo hali ikaanza kuchacha, na mtandao ukaanza kutafuta maana halisi ya ujumbe huo uliojificha.
Lakini kilichogeuza tahadhari hiyo kuwa kisanga cha mtandao ni fumbo lake lililotangulia: “What is nyevu… Something wet right…” 🤔💧
Ndani ya dakika chache, mitandao ikageuka darasa la kiswahili, maabara ya tafsiri na tamasha la vicheko – kila mtu alikuwa na version yake ya ‘nyevu’! 😂📱
🔸 Amos Tsui Chai
“Nyevuu Fondo ati inamaanisha noni 😅. Msamehe yuyu maana amalacho khondo nacho kinadima kumwika hafufu ela khamanya.”
🔸 Rehma Chikophe
“Anasema wewe na Chikuzeee ni customer wake wa mkorogooo 😂😂😂😂”
Muda huo mashabiki walikuwa tayari wameunganisha dots kuliko DCI – Kelechi, Chikuzee, na mkorogo! 🤣
🔸 Ammigo Dunga
“Namuona NYEVU akiandika na akifuta ila sijakufa moyo, nasubiri comeback yake. Something wet 🤣😂😂😂”
🔸 Bradley Pato
“Ati ‘something wet right?’ We Kelechi ni fala sana. Huwezi mwacha dadako kwa hali hiyo 😂😂😂 unataka ajinyonge??”
🔸 Khadijah Ali
“Kuna watu ni washari hapa duniani eti ‘something wet right’ 🤣🤣🤣🤣🤣”
Ikumbukwe kuwa Nyevu Fondo aliandika kwenye ukurasa wake akisema: “Huyu Kelechi Africana na Chikuzee Kenya tangu niwauzie mkorogo nkama wali-bleach hadi akili 🥱😂”
Entertainment
Chris Brown Akanusha Shtaka la Kumshambulia Producer kwa Chupa

Msanii nyota wa Marekani, Chris Brown, amekana mashtaka mawili mahakamani yanayohusiana na madai ya shambulio kwa kutumia chupa katika kilabu cha usiku jijini London miaka miwili iliyopita.
Nyota huyo mwenye umri wa miaka 36 anatuhumiwa kumsababishia mtayarishaji wa muziki majeraha ya mwili katika tukio ambalo waendesha mashtaka wamelieleza kuwa “halikuwa na uchochezi wowote”.
Pia anakabiliwa na shtaka la kumiliki silaha hatari — ambayo ni chupa ya kileo.
Mashtaka haya mawili yaliongezwa mwezi uliopita kwenye shtaka la awali, kubwa zaidi, la kujaribu kumsababishia mtu majeraha mabaya ya mwili (GBH), ambalo tayari Bwana Brown alilishatupilia mbali kwa kujitetea kuwa si kweli.
Chris Brown anatarajiwa kufikishwa mahakamani kwa kesi hiyo mwezi Oktoba mwaka 2026.
Waendesha mashtaka wamesema kuwa mhanga wa tukio hilo, Abraham Diaw, alikuwa amesimama kwenye baa ya kilabu cha usiku kilichopo eneo la Soho mnamo tarehe 19 Februari 2023, wakati Chris Brown alimpiga kwa chupa mara kadhaa.
Mwimbaji huyo alikamatwa mwezi Mei katika hoteli ya nyota tano iliyopo Salford, Greater Manchester, baada ya kurejea Uingereza kwa ajili ya maandalizi ya ziara yake ya muziki barani Ulaya.
Alizuiliwa korokoroni kwa takriban wiki moja kabla ya kuachiliwa kwa dhamana baada ya kukubali kulipa ada ya dhamana ya pauni milioni tano (£5m) kwa mahakama.
Ada ya dhamana ni kiasi cha fedha kinachowekwa kama dhamana ya kifedha kuhakikisha mtuhumiwa atarudi mahakamani kwa kesi yake. Brown anaweza kupoteza fedha hizo endapo atakiuka masharti ya dhamana, ambayo yaliendelezwa katika kikao cha mahakama siku ya Ijumaa.
Kwa mujibu wa masharti hayo, Chris Brown anatakiwa kuishi katika anwani iliyopo Uingereza akisubiri kesi hiyo, na aliamriwa kukabidhi pasipoti yake kwa polisi.
Hata hivyo, ameruhusiwa kuendelea na ratiba ya ziara yake ya kimataifa ya Breezy Bowl XX kwa masharti kwamba atakabidhi pasipoti kila anapomaliza safari, na kuirudishiwa anapohitaji kusafiri kwa ajili ya maonesho.
Katika wiki za hivi karibuni, Brown amekuwa akitumbuiza kwenye viwanja na kumbi mbalimbali za burudani kote Uingereza na Ulaya, na kumaliza burudani mjini Paris mwishoni mwa wiki iliyopita. Sehemu ya ziara hiyo inayofanyika Marekani Kaskazini inatarajiwa kuanza baadaye mwezi huu na kufikia tamati tarehe 18 Oktoba.
Kikao kingine cha mahakama kimepangwa kufanyika tarehe 24 Oktoba.
Chris Brown ni miongoni mwa wanamuziki wakubwa zaidi wa R&B nchini Marekani, akiwa mshindi wa tuzo mbili za Grammy na nyimbo 19 zilizofika katika nafasi 10 za juu kwenye chati za Uingereza, zikiwemo Turn Up The Music, Freaky Friday, With You na Don’t Wake Me Up.
Mshitakiwa mwenza, Omololu Akinlolu, raia wa Marekani mwenye umri wa miaka 39 anayefahamika kisanii kama HoodyBaby, naye pia alikana shtaka la kumsababishia mtu majeraha ya mwili. Awali, alikana pia shtaka la kujaribu kusababisha majeraha mabaya ya mwili.
Chanzo: BBC
Entertainment
Justin Bierber Arejea na Album Mpya ‘SWAGG’

Msanii nyota wa muziki wa kimataifa, Justin Bieber, hatimaye ameachia rasmi albamu yake mpya na ya saba kwa jina “Swag”, ikiwa ni albamu yake ya kwanza tangu mwaka 2021 alipotoa Justice. Albamu hii imetoka leo na tayari imeanza kutikisa majukwaa mbalimbali ya muziki duniani.
Swag imejumuisha mastaa kadhaa akiwemo Gunna, Sexyy Red, Cash Cobain, pamoja na wasanii wengine wa kizazi kipya.
Albamu hiyo ina jumla ya nyimbo 20 na tayari baadhi ya vibao kama “Go Baby”, “Soulful” na Butterflies “zimeanza kupokelewa vizuri kwenye mitandao ya Spotify, Apple Music na YouTube.
Hii ni mara ya kwanza kwa Bieber kuachia albamu tangu alipopata matatizo ya kiafya mwaka 2022 yaliyosababisha asitishe ziara yake ya kimataifa ya Justice World Tour ambayo ilikuwa iendelee hadi mwaka 2023.
Ziara hiyo ilisitishwa mnamo Septemba 2022 baada ya Bieber kupatwa na maradhi ya Ramsay Hunt Syndrome, ugonjwa uliomsababishia kupooza upande mmoja wa uso.
Kwa kipindi cha miaka minne bila kazi mpya, mashabiki wa Justin Bieber duniani wamekuwa wakimsubiria kwa hamu ujio wa kazi mpya kutoka kwake. Kupitia Swag, msanii huyo ameonyesha kurejea kwa nguvu na ubunifu wa hali ya juu, huku akiwa katika hali nzuri kiafya na kisaikolojia.
Taarifa na Francos Mzungu