Connect with us

News

Wataalam wa Uchumi wa Bahari washinikiza Viongozi kuwawezesha Wananchi.

Published

on

Wataalamu wa sekta ya uchumi wa samawati na maswala ya bahari hapa nchini wamesistiza haja ya serikali kuweka mazingira bora ya kubuni nafasi zaidi ya ajira ili kuinua uchumi wa bahari.

Mtaalam wa sekta hiyo Stanley Chai alisema uboreshaji wa mazingira ya sekta hiyo utachangia waekezaji zaidi kuekeza hapa nchini.

Chai alidokeza kuwa bahari hindi inafursa kubwa ya kuinua uchumi wa nchi kutokana na raslimali zinazopatikana bahari hindi.

“Nilazima tuweke mazingira yakuvutia meli nyingi, hii bahari yetu kuna mda ukiangalia kuna meli hamsini zinapita, tumekuwa tukishauri ulimwengu na kinachofanyika ni kuweka mazingira ya kuekeza upatikanaji wa samaki wa kiviwanda nchini, kama saa hii Kenya mtu akitaka liseni ya kwenda kuvua samaki kama hivi tuna tunamtoza dola elfu hamusini kwa mwaka”,alisema Chai.

Kuhusu swala la kudhibiti uingizaji wa bidhaa za samaki kutoka taifa la uchina katika soko la hapa nchini, mtaalam huyo alisema uhaba wa samaki hapa nchini umechangia uendelezaji wa biashara baina ya nchi hizo mbili ili kutosheleza lishe miongoni mwa jamii nchini.

 “Japan ndio walaji wakubwa wa samaki ulimwenguni, samaki wakiletwa hapa ndio wavuvi wetu watafaidi, wakati samaki wanapelekwa nje ujue samaki wetu wenye thamani ndio wanaenda nje na sisi tunakula tilapia ambao wameletwa kutoka huko, kama samaki wangekuwa wanatutosheleza hapa hakungekuwa na soko la wachina, lakini kwa sababu hawatutoshelezi ndio maana watu wamepata mwanya wa kuleta”, aliongeza mtaalam huyo.

Mtaalam wa maswala ya uchumi wa bahari Stanley Chai akipokezwa zawadi na Coco fm.

Wakati huo huo alishinikiza viongozi hapa nchini kutafuta ufahamu zaidi kuhusu maswala ya uchumi wa bahari sawa na kuweka mikakati ya kubuni nafasi za ajira ili kuwezesha wananchi kimaendeleo.

“Haieleweki kama wewe ni mbunge unasema utaendeleza eneo bunge lako na CDF ya shilingi milioni 170, hakuna maendeleo utaleta, kwa hivyo vingozi tunafaa kufikiria tofauti, tuje na njia mbadala ya kwamba tutabuni ajira na tutaleta utajiri watu wajitegemee na njia moja rahisi ni hii, sisi tunashukuru sana rais alisikiza akaelewa na kwa mara ya kwanza akaunda wizara nzima ya uchumi samawati, ninini tena unataka? Unataka kumlaumu rais tena?”, aliuliza Chai.

Tamko la mtaalam huyo linajiri wakati Kenya ikiadhimisha sherehe za miaka 62 za siku ya madaraka, ambazo ziliongozwa na rais William Ruto katika kaunti ya Homabay huku kauli mbiu ya maadhimisho ya sherehe za mwaka huu ikiwa ni “Uchumi sanawati na maswala ya bahari”.

Taarifa na Joseph Jira

 

Continue Reading
Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

News

Mahakama ya Malindi yawaachilia washukiwa 3 wa kesi ya Kwa Binzaro

Published

on

By

Mahakama Kuu ya Malindi imewaachilia washukiwa watatu wanaohusishwa na kesi ya mauaji ya halaki ya watu katika kijiji cha Kwa Binzaro eneo bunge la Magarini kaunti ya Kilifi.

Hakimu wa Mahakama hiyo Joy Wesonga aliagiza kuachiliwa huru kwa Safari Kenga Nzai, Gona Charo Kalama na Kahindi Kazungu Garama wote wakiwa wakaazi wa kijiji hicho cha Kwa Binzaro.

Watatu hao walikuwa wamekamatwa baada ya kudaiwa kuuza shamba la ekari tano kwa mshukuwa mkuu wa mauaji ya watu katika kijiji cha Kwa Binzaro Sherleen Temba Anido.

Hakimu Wesonga aliwaagiza washukiwa hao kuhakikisha wanasalimisha nakala za vitambulisha vyao vya kitaifa kwa idara husika, kuripoti kwa Naibu Chifu wa eneo hilo mara mbili kwa wiki pamoja na kujisalimisha kwa maafisa wa upelelezi wa kesi hiyo mara moja kila baada ya wiki mbili.

Miili iliyofukuliwa katika kijiji cha Kwa Binzaro 

Wakati huo huo upande wa mashtaka ukiongozwa na Naibu mkurugenzi wa mashtaka ya umma Jamie Yamina, uliomba kuwasilisha watu wengine wanne Mahakamani ikiwemo Jairus Otieno na mkewe Lilian Akinyi, Kahonzi Katana Karisa na Loise Zawadi waliojionda kama washukiwa na kugeuka kuwa mashahidi wa serikali.

Upande wa mashtaka pia uliaka kupewa siku 60 zaidi kuendelea kuzuiliwa kwa washukiwa wakuu Sherleen Temba Anido, James Kahindi Kazungu, Thomas Mukunwe na Kahidi Kazungu Garama katika kituo cha polisi cha Ngerenya, Kilifi, Watamu na Kijipwa ili kukamilisha uchunguzi wao kwani wanne hao wanakabiliwa na mashtaka ya itikadi kali, ugaidi, kujihusisha na uhalifu na kupanga mauaji.

Taarifa ya Mwahoka Mtsumi

Continue Reading

News

Chrispus aomba msahama bunge la kaunti ya Taita Taveta

Published

on

By

Mwakilishi wadi ya Bomani mjini Taveta kaunti ya Taita Taveta Chrispus Tondoo ameliomba bunge la kaunti hiyo msamaha kutokana na matamshi aliyoyatoa hapo awali akikashifu bunge hilo kwa madai ya kushamiri kwa visa vya ufisadi na utepetevu.

Tondoo akiomba msamaha katika bunge hilo alisema alitambua athari zilizosababishwa na matamshi hayo kwa wenyeji wa kaunti hiyo na bunge hilo, hali ambayo imemfanya kuchukua hatua hiyo ya kuomba msamaha.

Aidha Tondoo aliahidi kuliheshimu bunge hilo kwa mujibu wa kanuni na Sheria za bunge la kaunti ya Taita Taveta.

‘’Naomba msamaha kutokana na matamshi ambayo niliyatoa tarehe 2 na tarehe 3 mwezi wa Juni mwaka huu wa 2025 kwani hayakuwa yenye heshima kwa wenyeji wa Taita Taveta na bunge la kaunti’’, alisema Tondoo.

Tondoo alikuwa Mwakikishi wa wadi wa pili kuomba msamaha baada ya Mwakilishi wa wadi ya Kaloleni mjini Voi Ahmed Azari kuchukua hatua hiyo mwezi mmoja uliyopita.

Haya yalijiri baada ya kaimu spika wa bunge hilo Anselim Mwadime kuapa kuwachulia hatua za kisheria wanachama wanne wa bunge hilo, wawili wakiwa ni Tondoo na Azari ambayo tayari wameomba msamaha huku wawili wakiwa wamesalia bila kuomba msamaha.

Taarifa ya Janet Mumbi

Continue Reading

Trending