Sports
Wanariadha Kuvuna Panono Wakishinda Dhahabu Olimpiki

Serikali kupitia kwa Wizara ya Michezo imedokeza kwamba wanariadha wote wanaovunja rekodi na kufanya vizuri mashindano ya Olimpiki watavuna vinono haya ni kwa mujibu wa Waziri wa Michezo Salim Mvurya.
Waziri huyo aliyasema hayo wakati wa kupokea wanariadha bingwa wa olimpiki mita 1500 Faith Kipyegon na bingwa wa mitaa 5000 Beatrice Chebet baada ya kurejea nchini kutoka Eugene Oregon Marekani.
Kwa mujibu wa Mvurya mshindi wa tuzo la dhahabu Olimpiki sasa atakakua anapokea milioni 3 kutoka laki 750 huku mshindi wa fedha akipokea milioni 2 kutoka laki 500,000 naye wa shaba milioni moja.
Mwanariadha Kipyegon akivunja rekodi yake ya mitaa 1500 kwa muda wake bora wa dakika 3:48.68 huku Chebet akivunja rekodi kwa muda wa dakika 13:58.06.
Continue Reading
Sports
Manchester United Ndiyo mabingwa wa ‘PREMIERE LEAGUE SUMMER SERIES’

Manchester United imetwaa ubingwa wa kombe la ‘Premier League Summer Series’ kufuatia sare ya 2-2 dhidi ya Everton katika dimba la Mercedes-Benz, Atlanta, Georgia Marekani.
Michuano hiyo ya maandalizi ya msimu mpya ilishirikisha timu nne za Ligi Kuu England Man United, West Ham United, Everton na Bournemouth ambapo Mashetani hao Wekundu wamemaliza kileleni pointi 7 baada ya mechi tatu, wakishinda mechi mbili na kutoka sare mechi moja.
Kiungo Bruno Fernandes aliwaweka uongozini United dakika ya 18 kupitia mkwaju wa Penalti au Tuta kisha Iliman Ndiaye akisawazishia The Toffees dakika ya 40,United tena walichukua uongozi kupitia kwa kiungo mshambulizi Mason Mount dakika ya 69 kabila ya beki Ayden Heaven kujifunga dakika ya 75.
MSIMAMO:
1. Man UTD — mechi 3 — pointi 7
2. West Ham mechi 3 — pointi 6
3. Bournemouth mechi 3 — pointi 3
4. Everton mechi 3 — pointi 1
Sports
Stars yaanza vema CHAN kwa ushindi goli 1-0 dhidi ya DR-Congo

Timu ya Taifa ya Kenya (Harambee Stars) imechukua alama zote tatu kufuatia ushindi wa 1-0 dhidi ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo kwenye mchezo wa kwanza wa Kundi B wa kombe la Mataifa Afrika CHAN 2024 katika dimba la Moi Sports Centre, Nairobi.
Goli hilo la kipekee lilitiwa wavuni na kiungo mshambulizi Austine Odhiambo dakika 45 kipindi cha kwanza.
Rais William Ruto ambaye alifuatilia mechi hiyo uwanjani alitembelea kikosi katika chumba cha kubadilisha na kukabidhi ahadi yake ya shilindi milioni moja kwa kila mchezaji baada ya ushindi huo.
Stars wamekwea kileleni mwa kundi A na alama Tatu kundi ambalo pia lina Morocco,Zambia na Angola Mechi ijayo ya Stars ni dhidi ya Angola ni Agosti 7.