Business
Wakulima Rabai Wageukia Kilimo cha Viazi Vitamu Kufuatia Mvua Chache

Wakulima wanaoendeleza kilimo biashara kutoka rabai kaunti ya kilifi wamegeukia kilimo cha viazi vitamu.
Kulingana na wakulima hao msimu huu wa mvua chache viazi vitamu vinafanya vizuri ikilinganishwa na msimu wa masika.
Wakizungumza na cocofm wamesema kwa sasa kilimo cha viazi vitamu hakina hasara kwani kinachukua mda mfupi kuwa kukomaa na pia hakitumii maji mengi.
Aidha wamewashauri watu wengi kujihusisha na kilimo ili kujiinua kiuchumi.
“Kilimo cha viazi vitamu sai kinafanya vizuri kwani huwa havihitaji mvua nyingi na huu ni msimu wa mvua chache hivyo tunatarajia kufanya vizuri hata hivyo tunawaomba watu wengi kuingilia kilimo ili waweze kjiinua.”
Business
Wafanyabiashara Wadogo Kilifi Wakandamizwa na Nauli Ghali

Wafanyibiashara wanaotegemea huduma za tuktuk mjini kilifi kaunti ya kilifi wanalalamikia kukadiria hasara kutokana na hatua ya wahudu hao kupandisha nauli.
Wafanyibaisahara hao ambao ni wa kuhamahama wanasema kuwa hatua ya wahudumu wa tuktuk kuongeza bei ya nauli inawakagandamiza kwani hakuna pesa na kuongeza nauli inafanya maisha kuwa magumu.
Kulingana na wafanyibiashara hao imekuwa vigumu kwa wao kusafiri kutoka soko moja hadi nyingine kuendeleza biashara zao hali ambayo imeathiri maisha yao.
Wametolea wito wahudumu hao kuangizia upya swala hilo ili kuwasaidia wafanyibishara hao kuendeleza shughuli zao kwa urahisi.
Wakati huo huo wameitaka serikali na mamlaka ya udhibiti wa kawi kupunguza bei za mafuta .
Business
Idara ya Vijana Malindi na Magarini Yatishia Hatua Dhidi ya Walioshindwa Kulipa Mikopo

Idara ya vijana eneo bunge la Malindi na Magarini kaunti ya Kilifi inayataka makundi ya vijana, wanawake na walemavu yaliyopata mikopo ya hazina ya uwezo kulipa fedha za mikopo hiyo mara moja ili kuwezesha makundi zaidi kunufaika na hazina hiyo.
Kulingana na afisa msimamizi wa idara hiyo Juma Mtana Mwahunga, asilimia kubwa ya makundi yaliyokopa fedha hizo hayajarudisha hivyo kutatiza utekelezaji wa mpango wa hazina ya uwezo eneo hilo.
Mwahunga amekariri kuwa huenda makundi yaliyochukua mikopo hiyo hayakuzitumia fedha hizo kwa njia mwafaka hivyo kushindwa kulipa mikopo yao kwa wakati unaofaa ili kufanikisha mpango huo.
Afisaa huyo aidha amefichua kuwa jumla ya shilingi milioni 10 za hazina hiyo zilitolewa kupitia mikopo kwa makundi hayo huku milioni 3 pekee zikirudishwa kufikia sasa.