Connect with us

Sports

Wakenya Kuzindua Uhasama Mbio Za Oregon Prefontaine Classic

Published

on

Wanariadha nguli wa Kenya watatumia mbio za makala ya Oregon Prefontaine Classic kama mbio za majaribio kabila ya mbio za Dunia mjini Tokyo Japan badaye mwakani.

Bingwa wa Olimpiki mbio za mitaa 5000 na 10,000 Batrice Chebet anatarajiwa kuongoza wenzake katika mbio hizo wikendi hii ambapo chama cha riadha AK inatarajiwa kukiteuwa kikosi chake cha dunia.

Wanariadha wengine ambao wanarajiwa kutimka mbio hizo mjini Oregon Marekani ni pamoja na ;bingwa wa mbio za kilomita 10 Agnes Ngetich,bingwa wa zamani mbio za mitaa 10000 Caroline Nyaga,wengine ni pamoja na:  Margaret Akidor, Maurine Jepkoech, Janeth Chepngetich, Sarah Wanjiru, Caroline Kariba, na Hellen Ekalale.

Sheria za chama Raidha nchini AK zinaarifu kwamba washindi watakaomaliza nafasi za kwanza na ya pili wanafuzu moja kwa moja katika mashindano ya Dunia.

Continue Reading
Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Sports

Modric Rasmi Ametua Kwenye Kilabu Ya AC Milan

Published

on

By

Kilabu ya AC Milan imethibitisha kunasa huduma za kiungo mbunifu na mzee wa kazi Luka Modric kutoka Real Madrid kwa mkataba wa mwaka mmoja.

Raia huyo wa Croatia alipasi vipimo vya kimatibabu hapo jana kabila ya kuzinduliwa rasmi ugani San Siro

Mchezaji mwenye umri wa miaka 39 alijiunga na miamba wa uhispania mwaka 2012 akitokea katika kilabu ya Tottenham HotSpurs ambapo amekuwa na mafanikio makubwa mno ikiwemo kushinda mataji zaidi ya kumi na Los Blancos.

Modric ameshinda zaidi ya mataji 10 akiwa na kilabu hiyo ya Uhispania.

Continue Reading

Sports

Viwanja Vya Kenya Kasarani, Nyayo Tayari Kwa Kipute Cha Chan

Published

on

By

Mawaziri wawili waziri wa Michezo Salim Mvurya na waziri wa Usalama wa ndaani Kipchumba Murkomen wamethibitisha kwa pamoja viwanja vitakavyotumika kwa mtanange wa CHAN viko tayari.

Wakizungumza baada kuzuru uga wa Kasarani wawili hao wameweka wazi ubora wa viwanja hivyo viwili huku Mvurya akifichua kwamba kazi ya kuweka kanopi katika uga wa Nyayo kwa AFCON mwaka 2027 baada ya kukamilika kwa CHAN.

Kipute hicho kinangoa nanga mwezi ujao Agosti 2 ugani Benjamin Mkapa kabila ya fainali ugani Kasarani.

Continue Reading

Trending