Business
Wafugaji wa Kuku Jilore Wataka Mafunzo ya Kisasa Kutokomeza Hasara

Wafugaji wa kuku katika eneo la Jilore kaunti ya Kilifi wameitaka serikali ya kaunti kuwapa mafunzo ya kisasa kuwawezesha kuendeleza ufugaji ili kuepuka hasara ambazo wamekuwa wakishuhudia mara kwa mara.
Kulingana na Ishmael Menza wafugaji wengi hawana ufahamu kuhusu mbinu za kisasa za ufugaji hali ambayo inasababisha mapato duni.
Akizungumza na Coco FM, Menza anasema kuwa wafugaji hasa wadogo wamekuwa wakikadiria hasara kufuatia magonjwa yanashambulia kuku akisema wengi hajui aina za dawa ambazo wangetumia.
Hata hivyo Menza aimeitaka serikali kupunguza bei za dawa na chakula ili kuwasaidia wakulima hao wadogo kuendeza ufugaji bila changamoto.
Business
Mradi wa kiuchumi wa Dongo Kundu wavutia wawekezaji zaidi

Wawekezaji wa ndani na nje ya nchi wanaendelea kuonyesha nia ya kuekeza katika mradi wa kiuchumi wa dongo kundu kaunti ya Mombasa.
Mradi huo unaotarajiwa kuongeza uzalishaji katika viwanda na thamani ya bidhaa ndani ya nchi na nje, unatarajiwa kukamilika hivi karibuni.
Kampuni ya nishati kutoka China, Ruike Energy Group Limited, ni mwekezaji wa hivi karibuni kuonyesha nia ya kupata nafasi ndani ya eneo hilo la kiuchumi la Dongo Kundu kwa ajili ya kuanzisha kiwanda cha kusafisha mafuta.
Kulingana na halmashauri ya bandari nchini KPA hatua hiyo italeta faida Zaidi ikiwemo kubuni nafasi za ajira, ikuaji wa uchumi, upatikanaji wa vifaa vya baharini, na urahisi wa kufikia masoko ya kanda na ya kimataifa.
Taarifa ya Pauline Mwango
Business
KETRACO kuimarisha usalama wa chakula nchini

Shirika la usambazaji umeme nchini, KETRACO, limethibitisha dhamira yake ya kuimarisha usalama wa chakula, ukuaji wa kijani, na ushirikiano wa kieneo kupitia uekezaji mkubwa katika miundombinu ya umeme.
Katika maonesho ya Kimataifa ya kilimo ASK yanayoendelea kaunti ya Mombasa, KETRACO imeonyesha jinsi miundombinu yake ya umeme inavyowezesha kilimo cha kisasa na uzalishaji wa viwandani.
Kwa mujibu wa kaimu mkurugenzi mkuu, mhandisi Kipkemoi Kibias, KETRACO imekamilisha miradi 43 ya njia za kusafirisha umeme, huku mingine 29 ikitarajiwa kukamilika ifikapo mwaka 2028.
Kibias, alisema shirika hilo tayari limejenga zaidi ya kilomita elfu sita za njia za umeme wa msongo mkubwa, likiwa pia na vituo 46 vya kusambaza umeme na upanuzi wa mitambo 33.
Katika eneo la Pwani, Kibias alisema upanuzi wa mpango wa Green Energy Backbone umewezesha usambazaji wa kawi safi kwa asilimia 93, jambo lililopunguza utegemezi wa mafuta na kuchochea maendeleo ya biashara za kilimo, utalii na uchumi wa baharini.
Kibias alisema KETRACO inaendelea kuwekeza katika teknolojia za kisasa na kuunganisha Kenya na nchi jirani kupitia njia za kimataifa kama zile za Ethiopia, Tanzania na Uganda hatua zitakazowezesha biashara ya umeme Afrika Mashariki.
Taarifa ya Mwanahabari wetu
-
News20 hours ago
Mahakama ya Kilifi imetoa hukumu kwa wanaume 6 wanaokabiliwa na mashtaka ya unajisi
-
Sports19 hours ago
Kocha wa Uingereza Thomas Tuchel akataa madai ya “laana” huku akilenga kuvunja ukame wa miaka 60 wa mataji makubwa
-
News22 hours ago
Thoya: Serikali kuu iongeze mgao wa fedha kwa sekta ya Afya