News
Viongozi wa jamii ya Mijikenda wakosoa maandazili ya sherehe za Chenda chenda.

Baadhi ya viongozi wa jamii ya mijikenda eneo la pwani wamekosoa mpangilio wa sherehe za kitamaduni za jamii ya kimijikenda maarufu chenda chenda zilizofanyika jana Kaunti za Kilifi na Kwale.
Wakiongozwa na mwenyekiti ya baraza la jamii ya Chonyi Raphael Mwangala walisema msingi wa maandalizi ya sherehe hizo ni mshikamano ya jamii ya Mijikenda na wala sio mgawanyiko kama ilivyoshuhudiwa hapo jana.
Mwangala alisema taswira iliyojitokeza hapo jana hairidhishi kwa wamijikenda na inaonyesha hawana msimamo.
“Walioanzisha hii chenda chenda si lengo la kugawanyana, ni lengo la kuja pamoja, wengine wanachukua tu ni chenda chenda mijikenda waje wakae tu, lakini leo yule anaenda fanya Kwale, yule anaenda fanya wapi, hilo sio lengo, ningewasihi Mijikenda wenzangu, ngewasihi hata viongozi ambao wanajiita ni viongozi wa chenda chenda wafikirie lazima twende pamoja zi mambo ya kugawanyana”, alisema Mwangala.
Anadai sherehe hizo zimeingiliwa kisiasa akisistiza umuhimu wa kubuniwa kamati mpya ya jamii hiyo itakayohusisha mwakilishi wa kila kabila.
“Kwanza kamati ni wakina nani? Ni lazima kamati iuende mpya ya chenda chenda kwa kila mmijikenda awe mule ndani ya kamati ili wakipanga wawe wanaenda pamoja”, aliuliza Mwangala.
Baadhi ya watumbuizaji wa ngoma za kiasili katika sherehe za chenda chenda mjini Kilifi.
Kwa upande wake gavana wa kaunti ya Kilifi Gedion Mung’aro Mung’aro aliahidi kuunda kamati maalum itakayohusisha wazee wa Kaya ili kuangazia ulinzi wa misitu ya Kaya.
Akizungumza wakati wa sherehe hizo katika chuo kikuu cha Pwani, Gavana Mung’aro alisema kamati hiyo itahakikisha misitu ya kaya inazunghushiwa uwa ili kudhibiti uvamizi wa binadam.
Kauli ya gavana huyo ilijiri baada ya wazee wa Kaya kulalama kuwa misitu ya Kaya imekuwa ikisambaratika kutokana na uvamizi na kutatiza shughuli za mwendelezo wa mila na tamaduni za wamijikenda.
“Nitaunda kamati ya wazee wa Kaya tuangazia maneno ya misitu na mashamba ili kuwekewa ua ili itunzwe dhidi ya wavamizi,tunatengeneza kitengo cha vijana watyakaokuwa walinzi wa msitu kwa sababu tuiko na wizara hiyo ndani ya kaunti”, alisema Mung’aro
Kwa upande wake katibu katika wizara ya vijana na uchumi bunifu Fikirini Jacobs amesistiza jamii ya mijikenda hasa vijana kuzingatia umuhimu majukumu ya uongozi waliyonayo katika jamii.
Sherehe hizo ambazo ni makala ya nane kufanyika, ilifaa kufanyika kaunti ya Kwale kulingana na mpangilio wa awali wa kufanyika kile eneo la pwani japo kulifanyika mabadiliko siku za mwisho.
Mwenyekiti wa bodi ya barabara nchini Aisha Jumwa na gavana wa kaunti ya Kwale Fatuma Achani kwenye sherehe za Chenda chenda Kwale
Hatua hiyo ilikashifiwa na baadhi ya viongozi ambapo maandalizi mengine yalifanyika katika msitu wa Kaya Mtswakara kaunti ya Kwale ambapo mwenyekiti ya bodi ya barabara nchini Aisha Jumwa alihudhuria.
Taarifa ya Joseph Jira
News
Macharia: Jamii ya Kilifi kusini watapeliwa ardhi kufuatia ukosefu wa Elimu

Msaidizi wa Kamishna wa kaunti ya Kilifi eneo la Kilifi Kusini, Francis Macharia amesema ukosefu wa elimu umechangia kwa wanajamii wengi kaunti ya Kilifi kutapeliwa katika umiliki wa ardhi.
Akizungumza eneo la Vipingo, Macharia alisema kuwa wanajamii wengi hasa wazee wamekuwa wakitapeliwa mashamba yao kutokana na kukosa kisomo.
Macharia alisisitiza haja ya jamii kuzingatia elimu kwani visa vya ulaghai wa mashamba kutokana na ukosefu wa elimu vimekithiri mno hasa mashanani.
“Kuna baadhi ya vijana pia wamekuwa wakiwatapeli wazazi wao fedha za inua jamii pindi zinapotumwa, na hii imechangiwa na kutosoma wazee hao” aliongeza Macharia.
Macharia alisema wazazi pia wanapaswa kuwa mstari wa mbele kuhakikisha kuwa wanao wanapata elimu ipasavyo akisema kuwa eneo la Kilifi kusini limekuwa na visa vingi vya watoto wanaoacha shule na kuingilia vibarua.
Taarifa ya Hamis Kombe
News
Makalo atoa wito kwa serikali kuendeleza mpango wa ugavi wa chakula

Mwakilishi wa wadi ya Kasighau kaunti ya Taita Taveta Amos Makalo ametoa wito kwa serikali kuu kuendeleza mpango wa ugavi wa chakula cha msaada katika eneo hilo sawa na maeneo mengine kote nchini ili kunusuru maelfu ya wananchi wanaokabiliwa na baa la nja.
Makalo alisema chakula hicho ni kidogo mno kwani wananchi wengi wa Kasighau pamoja na maeneo mengine ya kaunti hiyo wanakabiliwa na baa la njaa.
Wakati huohuo Makalo alimshinikiza mwakilishi wa kike kwenye kaunti hiyo Lydia Haika kuishawishi serikali kuu kuikumbuka kaunti hiyo katika kupeana misaada mbalimbali ambayo itawafaidi wenyeji.
“Wananchi wanahangaika kutokana na njaa. Na kwasababu umetutembelea na mazuri leo wacha niombe kwamba hayo Mazuri yaendelee kwa muda huu ulio mbele yetu maana hali ni ngumu sana’’
Haya yanajiri huku Serikali ya kitaifa kupitia wizara ya huduma za kitaifa na mipango maalum ikiendeleza shughuli za usambazaji wa chakula cha msaada kwa wahanga wa baa la njaa kaunti ya Taita Taveta na maeneo mengine nchini.
Taarifa ya Janet Mumbi