Sports
Ureno Mabingwa Uefa Nations Ligi

Timu ya taifa la Ureno ndiyo mabingwa taji la Uefa Nations Ligi baaday ya kucharaza majirani wao Uhispania magoli 5-3 kupitia matuta au Penalti ukipenda
Hii baada ya timu zote kutoshana nguvu magoli 2-2 muda wa kawaida na ule ziada mechi iliopigwa ugani Allianz Arena.
Kiungo anayeiwindwa na Arsenal Martin Zubimendi aliwaweka uongozini The La Furia Rojas kwa faida ya Uhispania kunako dakika ya 21 kabila ya beki matata wa kushoto Nuno Mendes kuishazishia Ureno kunako dakika 26 kipindi cha kwanza.
Mshambulizi wa Real Sociadad Mikel Oyarzabal alirejesha tena mabingwa hao watetezi uongozini kunako dakika ya 45 kabila mshmabulizi nguli na mwamba wa miaka mingi Christiano Ronaldo kusawazishia Ureno dakika 61 kipindi cha pili.
Katika mechi ya kutafuta nafasi ya tatu Ufaransa walinyuka Ujerumani magoli 2-0.
Sports
Manchester United Ndiyo mabingwa wa ‘PREMIERE LEAGUE SUMMER SERIES’

Sports
Stars yaanza vema CHAN kwa ushindi goli 1-0 dhidi ya DR-Congo
