Business
Uhusiano wa Kibiashara kati ya Kenya na Ufaransa Waonyesha Ukuaji Chanya

Takwimu za kibiashara kati ya kenya na ufaransa katika kipindi cha miezi mitatu ya mwisho wa mwaka 2024 zinaonyesha kuwa ufaransa ilileta humu nchini bidhaa za thamani ya shilingi bilioni 6.5 na kuagiza bidhaa za thamani ya shilingi bilioni 5.7 kutoka humu nchini hali iliyoleta uwiano bora wa kibiashara kati ya nchi hizi mbili.
Nchi hiyo sasa inalenga kuimarisha zaidi uhusiano wake na kenya ambapo kenya imewaalika waekezaji zaidi kutoka nchini ufaransa kuekeza katika sekta kadhaa za kenya.
Waziri mwenye mamlaka makuu Msalia Mdavadi anasema ufaransa inalenga sekta za kawi, miundomsingi na tekinolojia ili kuongeza biashara kati yake na kenya.
Business
Kenya kuzindua utalii wa anga (Astro-tourisim)

Kenya itakuwa mwenyeji wa uzinduzi wa utalii wa anga(Astro-tourisim) katika kaunti ya Samburi Septemba 7, 2025, ikiwa ni sehemu ya juhudi za kuimarisha na kubadilisha aina za utalii nchini.
Uzinduzi huo unaendana sambamba na tukio la mwezi kupatwa maarufu kama Blood moon ambapo litaanza saa mbili na nusu usiku wa septemba 7, 2025, na kudumu kwa dakika 82.
Mpango huu wa kipekee unalenga kuifanya Kenya kuwa kivutio kikuu cha wapenzi wa sayansi ya anga na wasafiri wa kimataifa wanaopenda maajabu ya siri.
Kwa mujibu wa shirika la Magical Kenya, tajriba hii ya anga inalenga kutumia mazingira ya kipekee ya nchi kufungua ukurasa mpya na endelevu wa utalii.
Waziri wa utalii na wanyama pori Rebecca Miano atakuwa mgeni rasmi akiandamana na wageni wa kimataifa katika hafla hiyo itakayofanyika katika Sopa Lodge kwenye hifadhi ya kitaifa ya Samburu.
Taarifa ya Joseph Jira
Business
Mradi wa kiuchumi wa Dongo Kundu wavutia wawekezaji zaidi

Wawekezaji wa ndani na nje ya nchi wanaendelea kuonyesha nia ya kuekeza katika mradi wa kiuchumi wa dongo kundu kaunti ya Mombasa.
Mradi huo unaotarajiwa kuongeza uzalishaji katika viwanda na thamani ya bidhaa ndani ya nchi na nje, unatarajiwa kukamilika hivi karibuni.
Kampuni ya nishati kutoka China, Ruike Energy Group Limited, ni mwekezaji wa hivi karibuni kuonyesha nia ya kupata nafasi ndani ya eneo hilo la kiuchumi la Dongo Kundu kwa ajili ya kuanzisha kiwanda cha kusafisha mafuta.
Kulingana na halmashauri ya bandari nchini KPA hatua hiyo italeta faida Zaidi ikiwemo kubuni nafasi za ajira, ikuaji wa uchumi, upatikanaji wa vifaa vya baharini, na urahisi wa kufikia masoko ya kanda na ya kimataifa.
Taarifa ya Pauline Mwango