Sports
Uhispania Yaikomoa Ufaransa Uefa Nations Ligi.

UEFA NATIONS LEAGUE
Mabingwa watetezi wa taji la Uefa Nations Ligi Uhispania wameingia kwenye fainali ya taji hilo kwa kishindo Jumapili hii baada ya kunyuka Ufaransa magoli 5-4 hapo jana ugani Allianz Arena.
Winga matata wa Athletico Bilbao Nico Williams aliweka uongozini Uhispania dakika ya 22 kabila ya mshambulizi wa Arsenal Mikel Merino kuweka la pili dakika ya 25 kipindi cha kwanza.
La Furia Roja aliendeleza walipoachia kipindi cha kwanza katika kipindi cha pili huku winga wa Barcelona Lamine Yamal akiweka chuma ya tatu dakika ya 54,na lingine dakika ya 67 kabila ya Pedri kuweka la nne dakika ya 55 na kufanya mambo kuwa magoli 5-0
Hata hivyo Ufaransa walirejea kwa kishindo wakijipatia magoli kupitia Kyllian Mbappe dakika ya 59 naye Ryan Cherki dakika ya 79 Randal Kolo Muani dakika ya 93 uhispania pia wakijifunga kupitia beki Vivian.
Fainali ya Uefa Nations ligi ni kati ya Uhispania na Ureno jumapili saa nne usiku.
Sports
Manchester United Ndiyo mabingwa wa ‘PREMIERE LEAGUE SUMMER SERIES’

Sports
Stars yaanza vema CHAN kwa ushindi goli 1-0 dhidi ya DR-Congo
