Connect with us

News

Tiketi za Mashemeji Debi Zimeanza Kuuzwa

Published

on

Debi la mashemeji kati ya mahasimu wa tangu jadi kilabu ya Gor Mahia na Afc leopards siku ya jumapili kuendelea kama ilivyopangwa haya ni kwa mujibu wa waandalilizi wa mtananga huo Gor.

Tiketi za mchuano huo tayari zimetolewa ambapo mashabiki wa kawaida wanalipia ada ya shilingi shs.300 na mashabiki mashuhuri shs.500.

Awali kulikua na hali ya sintofahamu kuhusiana na ubora wa uwanja wa Kasarani ambao bado unakarabatiwa kuanda mechi ila wakilishi wa kogalo wamepata hakikisho kutoka kwa wasimamizi wa uga huo.

Katika mechi ya mkondo wa kwanza timu hizo mbili ziliisha sare tasa ugani Nyayo,Kogalo kwa sasa ni ya tatu ligini na alama 51 huku Afc Leoprads wakiwa ya sita na alama 42 kutokana na mechi 29.

Continue Reading
Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

News

Mahakama kuu yatupilia mbali ombi la Gachagua

Published

on

By

Mahakama kuu imetupilia mbali ombi la pili la aliyekuwa Naibu Rais Rigathi Gachagua la kutaka jopo la majaji watatu wanaosikiliza kesi ya kupinga kubanduliwa wake mamlakani kuzuiliwa kuskiza kesi hiyo. 

Gachagua alisema kwamba majaji hao watatu akiwemo Jaji Eric Ogola, Anthony Mrima na Fridah Mugambi wanafaa kuondolewa kwenye kesi hiyo kwa misingi kwamba uteuzi wao haujazingatia sheria.

Mahakama hiyo ilitupilia mbali ombi hilo, na kusema kwamba jopo hilo la majaji watatu liliteuliwa na Jaji mkuu Martha Koome kwa kuambatana na sheria na kanuni za idara ya Mahakama.

Mahakama imeshikilia kwamba jopo hilo la majaji wa Mahakama kuu litaendelea kusikiliza kesi hiyo hadi wakati wa kutoa uamuzi kwa kuzingatia sheria, na kanuni za idara ya Mahakama pamoja na Katiba ya Kenya.

Mahakama hiyo pia ilitupilia mbali ombi la Mwanaharakati Fredrick Mula ambaye alitaka kubadilishwa kuwa mlalamishi katika kesi nne za kuondolewa mashtaka dhidi ya aliyekuwa Naibu Rais Rigathi Gachagua ambazo alikuwa amewasilisha awali na kisha kutaka kujiondoa.

Taarifa ya Mwahoka Mtsumi

Continue Reading

News

Wazee wa Kaya wanataka bunge kupitisha sheria kudhibiti mauaji ya wazee

Published

on

By

Muungano wa Wazee wa Kaya kaunti ya Kilifi umeitaka serikali kuu kupitia bunge la kitaifa kubadilisha sheria ya mwaka wa 1926 kuhusu uchawi ili kuwezesha utamaduni kudhibiti mauaji ya wazee yanayoendelea kushuhudiwa kaunti ya Kilifi.

Wakiongozwa na Stanley Kahindi Kiraga wamesema kuwa sheria hiyo imechangia pakubwa mauaji ya wakongwe Kilifi kutokana na swala kuwa haitambui uwepo wa uchawi na jinsi ya kuudhibiti.

Kiraga sasa anasema ni sharti sheria hiyo iondolewe au ifanyiwe ukarabati bungeni hali itayopelekea uchawi kudhibitiwa kupitia mila na utamaduni.

“Vijana wanaowaua wazee wakiwasingizia kuwa wachawi wanazidi kuongezeka na kwa sababu hakuna sheria ya moja kwa moja ya kuwashtaki na kuwafunga” amesema Kiraga akieleza kusikitishwa kwake na ongezeko la magenge ya vijana wanaolipwa kutekelezwa mauaji ya wazee kwa shutuma za uchawi.

Taarifa ya Hamis Kombe

Continue Reading

Trending