Connect with us

Sports

Starlets Uwanjani Tena Amunyolet Akilenga Mfungaji Bora

Published

on

Kiungo mshambulizi wa Harambee starlets Martha Amunyolet amesema kwamba analenga kuwa mfungaji bora kwenye Makala yam waka huu ya CECAFA nchini Tanzania

Kiungo huyo wa Kilabu ya Vihiga Queens ambaye saa hii ana magoli 3 ana amini atafunga zaidi katika mechi zijazo dhidi ya Sudan Kusini na Twiga Stars ya Tanzania.

“Niko hali nzuri na nilifunga Burundi magoli 2,pia Uganda nilijua nitafunga pia na sasa malengo yangu ni kufunga magoli mengi na kuwa mfungaji katika mashindano haya ndio nawazia si lingine.”

katika ratiba za leo Kenya vs S.Sudan 4pm

Tanzania vs Uganda 7pm

Continue Reading
Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Sports

Liverpool Yakubaliana Dili Ya Kerkez

Published

on

By

Kilabu ya Liverpool imekubaliana na AFC Bournemouth kuhusiana na uhamisho wa pauni milioni 4o kwa beki Milos Kerkez raia wa Serbia.

Tineja huyo anatarajiwa kuwasili Liverpool muda wowote kufanyiwa vipimo vya kimatibabu na kumwaga wino mkataba wa miaka mitano na mabingwa hao wa ligi kuu Uingereza.

Mchezaji huyo alikua nguzo muhimu kwa kilabu ya Bournemouth wakimaliza kumi bora akichangia magoli matano na kufunga mawili,anakua sajili wa tatu kwa kocha Arne Slot kwenye kilabu hio.

The Reds wakiwa wametumia pauni milioni 116 kumpata kiungo Florian Wirtz,pauni milioni 31 kupata Jeremie Frimpong.

Continue Reading

Sports

Starlets Kucheza Fainali Ya CECAFA Dhidi Tanzania

Published

on

By

Kikosi cha soka akina dada kushuka dimbani kucheza dhidi ya Twiga Stars Ya Tanzania kwenye fainali ya kipute cha CECAFA Afrika Mashariki ugani Azam Sports Complex.

Vipusa wa kocha Beldine Odemba wameshinda mechi zote tatu ikiwemo kuwalaza Sudan Kusini magoli 4-0 mechi ya siku ya Alhamisi huku wakiwa wamekusanya alama 9 sawa na wenyeji Tanzania kwenye mashindano ya mwaka huu.

kwa mujibu wa mwalimu huyo wanatarajia mechi ngumu dhidi ya wapinzani wao kwani wako nyumbani na timu bora pia.

“Tuko tayari kwa mechi ya mwisho ambayo pia ni fainali kila mmoja anajua tumekua vizuri katika mashindano haya ila Tanzania ni mpinzani mkubwa katika fainali ya leo kwa sababu pia hawajapoteza mechi kama sisi.”

Mechi hiyo inangoa nanga saa 12.00 jioni.

Continue Reading

Trending