Connect with us

News

Serikali yabaini ulaghai uliofanywa katika NHIF

Published

on

Wizara ya Afya nchini imedai kuwa kumekuwepo na ulaghai mkubwa katika mfumo wa zamani wa bima ya afya ya NHIF.

Waziri wa Afya, Aden Duale alisema kuwa zaidi ya visa milioni 3 vya ada hewa ya matibabu, vimebainika wakati wa shughuli ya uhamisho wa huduma kwenda kwa bima ya afya ya jamii kwa wote (SHA).

Waziri Duale, alidokeza kuwa uchunguzi unaendelea ili kuwatambua wahusika wa sakata hiyo na kuwachukulia hatua kali za kisheria.

Akizungumza mbele ya kamati ya bunge la kitaifa kuhusu afya, waziri Duale alifichua kuwa kuna madai ya udanganyifu unaotekelezwa na baadhi ya hospitali zinazolenga kufyonza fedha kwa njia isiyo halali kutoka kwa bima ya SHA.

Duale aalisema kuna ushahidi kuwa baadhi ya hospitali hudai kutekeleza upasuaji ambao haukufanyika, na hata kuwasilisha madai ya uongo kuhusu watu waliolazimishwa kutoa damu bila sababu za kiafya.

Taarifa ya Mwanahabari wetu

Continue Reading
Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

News

Anselim, ashutumu utovu wa usalama Taita Taveta

Published

on

By

Kaimu Spika katika bunge la kaunti ya Taita Taveta Anselim Mwadime alieleza kusikitishwa na mauaji ya mhudumu mmoja wa bodaboda aliyeuliwa na kisha pikipiki yake kuchukuliwa katika eneo la chuo kikuu cha Taita Taveta.

Mwadime alisema kuna baadhi ya abiria ambao ni wahuni hubebwa na kisha kuwashambulia wahudumu wa pikipiki hadi kuwaua au hata kutoweka na pikipiki.

Aidha, Mwadime alisema kama viongozi wa kaunti ya Taita Taveta hawataruhusu visa hivyo kuendelezwa katika kaunti hiyo.

Vilevile, Mwadime aliishinikiza idara ya usalama kwenye kaunti ya Taita Taveta kuwajibika ipasavyo ili kudhibiti visa vya utovu wa usalama katika sekta ya bodaboda na wanaohusika wakabiliwe kisheria.

“Hili jambo linafaa kufuatiliwa kwa undani. Na tunalilaani vikali sisi kama viongozi wa Taita Taveta’’ alisema Mwadime.

Taarifa ya Janet Mumbi

Continue Reading

News

Viongozi wahimizwa kushirikiana kubuni ajira kwa vijana

Published

on

By

Mwakilishi wa wadi ya Sabaki eneo bunge la Magarini kaunti ya Kilifi Rose Baraka alitoa wito kwa viongozi wa kaunti ya Kilifi kushirikiana na mashirika ya kijamii pamoja na wawekezaji katika kaunti ya Kilifi ili kudhibiti changamoto za ukosefu wa ajira miongoni mwa vijana.

Rose alisema hatua hiyo itasaidia pakubwa kuwaepusha vijana kujiingiza kwenye utumizi wa mihadarati sawa na uhalifu.

Akizungumza wakati wa kikao kilichowaleta pamoja maafisa wa shirika la SHOFCO pamoja na wakaazi wa Sabaki, Rose aliahidi kushirikiana na mashirika mbalimbali ya kijamii katika juhudi za kuwasadia wananchi kujiendeleza kupitia mpango wa ajira.

“Vijana ni wengi, kazi ni kidogo. Sisi kama viongozi tunastahili kutia bidii kutafuta haya mashirika ili tuangalie vijana wetu wasaidika vipi’’ alisema Rose Baraka.

Kwa upande wake Afisa wa Shirika la SHOFCO eneo la Magarini Kelvin Mtawali Karisa aliupongeza ushirikiano wa mwakilishi wa wadi huyo na shirika hilo na kuwataka vijana kujiunga kwenye makundi mbalimbali ili waweze kupata mikopo ya kujiendeleza kimaisha.

Taarifa ya Janet Mumbi

Continue Reading

Trending