Connect with us

Sports

Serani Waahidi Kutetea Ubingwa Mashindano Ya Shule ya Upili

Published

on

Mabingwa watetezi wa soka kwa shule za upili kaunti ya Mombasa upande wa wavulana, shule ya upili ya SERANI walianza vyema kampeni ya kutetea taji lao kwa kupata ushindi katika mechi zao zote za makundi.

Katika mechi ya kwanza waliicharaza shule ya upili ya Kajembe 3-0 na Kisha wakawageukia vijana wa shule ya upili ya Khadija na kuwalaza mabao 2-0.Katika mechi zingine, St Charles Lwanga wameona moto kwa kutandikwa 1-0 na Tononoka, Kisha Khadija wakavuna ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Shikaadabu, Moi Forces Academy wakiwachapa St Charles Lwanga 2-0 na Kajembe wakatoka 1-2 dhidi ya Shikaadabu.

Shule ya upili ya Mwakirunge bahati haikuwa upande wao kwani baada ya kupokea kichapo cha mabao 5-0 kutoka kwa Moi Forces katika mechi ya kwanza,   hawakuweza kurejea uwanjani kwa kipindi cha pili cha mechi yao ya pili dhidi ya Tononoka ambapo tayari walikuwa wamechapwa magoli 3-0 katika kipindi cha kwanza, wakieleza kuwa hatua hiyo imetokana na wachezaji wengi kupata majeraha wakiwa uwanjani na kubaki na wachezaji 6 pekee.

MOMBASA COUNTY KSSSA DAY 2 FIXTURES

GIRLS SOCCER  –  8:00 AM
Changamwe Girls vs Mwakirunge – Tudor Day
Mekatilili vs Moi Forces Girls – Makande
Kaa Chonjo vs Mishi Mboko – Tudor Pry
Kajembe vs Mama Ngina – RG Ngala
BOYS SOCCER  –  10:00 AM
Tononoka vs Moi Forces Boys – RG Ngala
Mwakirunge vs St Charles – Tudor Pry
Khadija vs Kajembe – Makande Primary
Serani vs Shikaadabu – Tudor Day
Continue Reading
Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Sports

Liverpool Yakubaliana Dili Ya Kerkez

Published

on

By

Kilabu ya Liverpool imekubaliana na AFC Bournemouth kuhusiana na uhamisho wa pauni milioni 4o kwa beki Milos Kerkez raia wa Serbia.

Tineja huyo anatarajiwa kuwasili Liverpool muda wowote kufanyiwa vipimo vya kimatibabu na kumwaga wino mkataba wa miaka mitano na mabingwa hao wa ligi kuu Uingereza.

Mchezaji huyo alikua nguzo muhimu kwa kilabu ya Bournemouth wakimaliza kumi bora akichangia magoli matano na kufunga mawili,anakua sajili wa tatu kwa kocha Arne Slot kwenye kilabu hio.

The Reds wakiwa wametumia pauni milioni 116 kumpata kiungo Florian Wirtz,pauni milioni 31 kupata Jeremie Frimpong.

Continue Reading

Sports

Starlets Kucheza Fainali Ya CECAFA Dhidi Tanzania

Published

on

By

Kikosi cha soka akina dada kushuka dimbani kucheza dhidi ya Twiga Stars Ya Tanzania kwenye fainali ya kipute cha CECAFA Afrika Mashariki ugani Azam Sports Complex.

Vipusa wa kocha Beldine Odemba wameshinda mechi zote tatu ikiwemo kuwalaza Sudan Kusini magoli 4-0 mechi ya siku ya Alhamisi huku wakiwa wamekusanya alama 9 sawa na wenyeji Tanzania kwenye mashindano ya mwaka huu.

kwa mujibu wa mwalimu huyo wanatarajia mechi ngumu dhidi ya wapinzani wao kwani wako nyumbani na timu bora pia.

“Tuko tayari kwa mechi ya mwisho ambayo pia ni fainali kila mmoja anajua tumekua vizuri katika mashindano haya ila Tanzania ni mpinzani mkubwa katika fainali ya leo kwa sababu pia hawajapoteza mechi kama sisi.”

Mechi hiyo inangoa nanga saa 12.00 jioni.

Continue Reading

Trending